Home BUSINESS NAIBU WAZIRI MABULA APONGEZA UBUNIFU WA WAJASIRIAMALI, ATEMBELEA BANDA LA TOBI PRODUCTS...

NAIBU WAZIRI MABULA APONGEZA UBUNIFU WA WAJASIRIAMALI, ATEMBELEA BANDA LA TOBI PRODUCTS SABASABA

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla (Kulia) Akizungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Tobi Products Agatha Laizer (Kushoto) alipofika kumtembelea kwenye Banda lake Katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Angela Mabula  namna ambavyo anatayarisha Bidhaa yake ya Siagi ya Karanga wakati Naibu Waziri huyo alipofika kwenye Banda la Mjasiriamali huyo kujionea shughuli zake na kumpongeza.(PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabulla akitia saini kwenye kitabu maalum cha wageni katika Banda la Kampuni ya  Tobi Products kwenye maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Tobi Products Agatha Laizer (wa kwanza kulia) akiwa na Ofisa Mauzo wa Kampuni hiyo (kulia kwake) wakimuhudumia mteja aliyefika kwenye Banda lao kuona na kununua Bidhaa ya Siagi ya Karanga iliyotokea kupendwa na kuvutia watu wengi kwenye Maonesho ya Sabasaba. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Tobi Products Agatha Laizer akipanga vizuri Bidhaa zake tayari kwa kuuzwa. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Tobi Products Agatha Laizer (Kushoto)  Sophia Amon (kulia) kutoka Kampuni ya Halisi Product. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).

 Na; Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.

Naibu waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabulla amempongeza mjasiriamali Aghatha laizer kwa kuwa mbunifu kwa kutengeneza bidhaa zenye ubora  kwa kutumia malighafi za nyumbani kwa maendeleo ya watanzani wenyewe.

Naibu waziri huyo ambaye alipata fursa ya kufika kwenye maonesho ya sabasaba na kupata fursa ya kuzungukia baadhi ya mabanda mbalimbali huku akuionyesha kufurahishwa na namna wanawake walivyojitokeza kwa wingi kuleta bidhaa zao kwenye maonyesho hayo.

Naye mjasiriamali huyo ambae pia ni mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni ya Tobi products yenye makao yake ukonga ndani ya halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Aghatha Laizer amesema kuwa anajisikia vizuri kutembelewa na naibu waziri Mabula na angalau kumpongeza kwa ubunifu wake wa kutengeza siagi ya karanga ambayo imesindikwa kwa viwango vyenye ubora.

“Nimefurahi kwa kwakweli na nimejisikia mwenye bahati hasa kumuona waziri kwenye banda langu lakini pia ameniungisha bidhaa zangu na kunipa hongera na moyo katika kile ambacho nakifanya hivyo nawaomba watanzania wengine kufika kwenye banda langu ambalo lipo hapa kwenye jengo la VIP na linatazamana na wizara ya madini.”amesema Aghatha.

Amesema kuwa kwasasa wanapatikana na kwenye maonyesho ya sabasaba hadi pale yatakapomalizika na baada yahapo ofisi zao zipo ukonga Mombasa  hivyo wananchi watembelee kwenye banda lake kupata huduma bora na bidhaa zilizotengenezwa kwa kiwango bora kabisa Siagi za karanga ambazo unaweza  kuungia mboga ,kupaka kwenye mkate na mambo mengine mbalimbali na inaleta hamu ya kula kila wakati. 

Aghata ameongeza kuwa mbali na bidhaa hiyo lakini pia unga halisi wa lishe pamoja na viungo mbaalimbali vya chakula na chai ambavyo vimewekwa kwenye vifungashio bora waje wajipatie bidhaa hizo kwa ajili ya kuimarisha afya zao. 

Naye Sophia Amon kutoka kampuni ya Halisi Product amesema kuwa bidhaa zingine ambazo wanazo katika maonyesho hayo ni Soya Drinks ,Ginder ,Mdarasini ,Tea masala ,Asali pamoja na unga wa uji kwa ajili ya lishe huku akiwataka wananchi kusogelea kwenye banda lao kujipatia viungo hivyo pamoja na bidhaa zingine.

 

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here