Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato akimsikiliza Mwanji Mbaka Mhandisi Mjenzi Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) wakati alipokuwa akielezea maendeleo ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere Hydro Power unaojengwa Rufiji katika mikoa ya Pwani na Morogoro wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TANESCO katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato akihoji jambo kwa Mwanji Mbaka Mhandisi Mjenzi Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) wakati alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi huyo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaojengwa Rufiji katika mikoa ya Pwani na Morogoro wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TANESCO katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato akimsikiliza Mwanji Mbaka Mhandisi Mjenzi Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) wakati alipokuwa akimfafanulia zaidi maendeleo ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere Hydro Power unaojengwa Rufiji katika mikoa ya Pwani na Morogoro wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea banda la TANESCO katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato akimsikiliza Bw. Agustine Kasale afisa Mawasiliano Kampuni ya Uendelezaji Joto Ardhi Tanzania (TGDC) wakati alipotembelea banda la TANESCO kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato akimsikiliza Mhandisi wa Mitambo kutoka Shirika la (TGDC) kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato akioneshwa mtambo uliobuniwa na Amani Christopher Mhandisi wa Mitambo kutoka Shirika la (TGDC) kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
DAR ES SALAAM.
Naibu Waziri Wizara ya Nishati Mh. Stephen Byabato amesema Mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere Hydro Power Project JNHPP unakwenda kutatua changamoto nyingi za maendeleo kwa watanzania katika suala zima la upatikanaji wa umeme wa Uhakika.
Naibu Waziri Byabato ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la TANESCO kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Julai 06, 2021 na kujionea ubunifu wa wahandisi watanzania ambao wamebuni mfano wa mradi huo na kuuleta kwenye maonesho hayo kwa ajili ya kuwaonesha wananchi kile kinachoendelea huko Rufiji.
Amesema kwa sasa tunazalisha Megawati moja ya umeme wa maji kwa shilingi 36 wakati umeme wa mafuta tunazalisha megawati moja kwa zaidi ya shilingi 500 hivyo utaona kabisa kuwa umeme wa maji ni wa bei rahisi kabisa.
“Na ndiyo maana umeme wa vijijini kwa sasa kuunganisha ni shilingi elfu 27.000 tu kitu ambacho kinarahisisha maisha ya watanzania kwa sababu umeme ndiyo kila kitu katika maendeleo,”. amesema Waziri Byabato.
Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kauli mbiu yake ya “Kazi Iendelee” hii inamaanisha kwamba mradi huu wa umeme ni muhimu na utaliletea taifa faida kubwa katika suala zima la maendeleo ya viwanda.
Amesema kukamilika kwa bwawa hili itakuwa ni faraja kubwa kwa sababu faida za mradi huu tutakuwa tumeongeza umeme wa gharama na nfuu kwa watanzania na kwa majirani zetu hapa nchini na usambazaji wa umeme kwa vijijini Rea itakuwa chini kabisa.