Home ENTERTAINMENTS MISS IFM KUCHUANA KESHO J.MOSI JULAI 10-2021

MISS IFM KUCHUANA KESHO J.MOSI JULAI 10-2021

NA: MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM.

WALIMBWENDE 20 wanatarajiwa kuchuana vikali Julay 10 katika jukwaa la kuwania taji la Miss IFM 2021,  City Gadeni Dar es Salaam.

IFM ni miongoni mwa chuo ambacho kimekuwa kikitoa warembo amba wanafanya vizuri katika mashindano ya ngazi za juu ya urembo akiwemo Dayana Edward miss Tanzania 2016.

Akizungumza na gazeti hili mratibu washindano hilo Sixtus Kamanda, amesema washiriki wamejipanga kutoa shoo kubwa ambayo ita ambatana na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali

“Washiriki wetu waneingia kambini kwa muda wa mwezi mmoja wamejifua kikamilifu na wote wana vigezo vya kunyakuwa taji niwaombe wadau kujitokeza kwa wingi siku hiyo,” alisema Kamanda.

Kwa upande wa burudani atakuwepo mshindi wa Bongo Star seach 2020, Yuzzo na wasanii wengine pamoja na mastaa mbalimbali katika tasia ya mitindo akiwemo Ally Rehmtula na miss Tanzania 2020 Rose Manfere.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here