Mbunge wa Jimbo LA Segerea Bonah Ladslaus Kamoli (Kulia wa pili)akipata maelezo kutoka kwa Afisa Tarura Wilaya ya Ilala Sililo Joseph leo Julai 26/2021 kusiana na maendeleo ya Daraja la Kipunguni Banana ambalo limegharimu Shilingi milioni 250 (Kushoto kwa Mbunge)Diwani wa Kipawa Aidan Kwezi na Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilala MH,Cheka .katika ziara ambayo imeandaliwa na Mbunge kukagua miradi ya Jimbo la Segerea(PICHA NA HERI SHAABAN)
MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Serikali ambayo itajengwa Liwiti .
Mbunge Bonah aliyasema hayo Dar es Salaam Jana katika mwendelezo wa ziara zake za kutembelea miradi ya serikali na kutatua kero za Wananchi.
“Kata ya Liwiti miongoni mwa kata iliyokosa shule ya sekondari miaka yote naipongeza Serikali yangu kunipatia fedha sekta ya Elimu iweze kukua tunatarajia kuanza ujenzi wa Shule mpya ili watoto wasiende mbali “ alisema Bonah
Mbunge Bonah alisema ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara zake amekua akiifanya katika Jimbo hilo, ambapo leo ametembelea Kata ya Segerea, Liwiti, Vingunguti pamoja na Kipawa na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo Ujenzi wa daraja barabara ya Banana kitunda, barabara ya Vingunguti Barakuda pamoja na taa za stendi ya Segerea.
Aidha, amesema kuwa, ameridhishwa na Ujenzi wa miradi ya Maendeleo katika Jimbo hilo ambapo amesema miradi hiyo inatekelezwa kwa pesa za Serikali kuu pamoja mfuko wa Jimbo.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Liwiti Arafa Shamna amesema kuwa, kuwepo kwa shule ya Sekondari katika kata hiyo itakua msaada mkubwa na kupunguza adha ya usafiri wanayoipata wanafunzi kwenda umbali mrefu ikiwemo Kata ya Chanika, Zingiziwa, Minazi Mirefu pamoja na Segerea.
Naye, Diwani wa kata ya Liwiti Alice Mwangomo amesema anaishukuru Serikali kwa kuingalia barabara ya Vingunguti barakuda kwani barabara hiyo inaunganisha wakazi wa Segerea na Vingunguti na Maeneo ya jirani.
Katika hatua nyengine, Diwani wa Kata ya Kipawa Aidan Kwezi amesema kuwa kata hiyo inatarajiwa kuwa na miradi mingi ya Maendeleo ikiwemo ujenzi wa daraja katika barabara ya Banana kitunda ambao umekamilika kwa asilimia kubwa.
“Barabara ya Uwanja Ndege , Karakata nayo pia inatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi utaanza muda si mrefu kwani wananchi wamekua wakipata shida kubwa kutokana na barabara hiyo sio rafiki kwao”alisema Aidan.
Aidha, Mtendaji wa Kata ya Segerea Eligius Mulokozi alisema mpaka sasa kata hiyo imeshapokea zaidi ya sh, mill 60 kwa ajili ya miradi ya Maendeleo ikiwemo taa za stendi ya Segerea,ukarabati wa barabara pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa upande wa sekta ya elimu.
Mwisho