Na: Heri Shaaban, DAR ES SALAAM.
MBUNGE wa jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli amelizishwa na utekekezaji wa Miradi ya maendeleo jimbo la Segerea Wilayani Ilala .
Mbunge Bonah aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika ziara yake ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo ipo jimboni humo.
Akizungumza katika ziara hiyo ya kutembelea kata ya Kinyerezi,Tabata na Buguruni na Makatibu wa Jimbo alisema dhumuni la ziara hiyo kuangalia utekelezaji wa miradi ya serikali ambayo inajengwa na mingine hipo hatua za mwisho
“Nimeanza ziara endelevu katika jimbo la Segerea ya kutatua kero na kuangalia utekelezaji wa miradi ya serikali ambayo inajengwa naomba wananchi wa Segerea mtunze miradi yenu ” alisema Bonah.
Bonah alimpongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa kifanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa jimboni humo ikiwemo miradi ya DMDP kituo cha Daladala Kinyerezi, na Barabara ya Gongolamboto yenye thamani ya shilingi bilioni. 17 .
Katika ziara hiyo Bonnah pia amepata nafasi ya kuzungumza na wananchi mbalimbali ambapo katika Mtaa wa Kifuru Kata ya Kinyerezi wameomba ujenzi wa barabara ya NST Bangulo uharakishwe kwani wamekuwa wakipata adha kubwa hasa wakati wa mvua.
Injinia Mahobe Abdul akimweleza mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli, maendeleo ya ujenzi wa stendi hiyo.
Naye Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Leah Ng’itu, ameomba wasaidiwe barabara za ndani kwa kuweka vifusi pamoja na kukarabati maeneo korofi kwenye barabara za lami.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buguruni, Busoro Pazi, amesema ujenzi wa mfereji katika Mtaa wa Mvinjeni utakuwa ni suluhisho la kero ya mafuriko katika eneo hilo.
“Tunamshukuru mbunge wetu kwa juhudi kubwa alizozifanya kuhakikisha katika Mtaa wa Mivinjeni mfereji huu unajengwa, changamoto ya maji kutoka katika Mto Msimbazi kwenda kwenye makazi ya wananchi ilikuwa ni kubwa sana lakini kupitia ujenzi wa mfereji kero hii itaisha kabisa,” alisema Pazi.
Diwani Busoro Pazi aliwataka Wananchi kulipa kodi kila wakati ili Serikali iweze kupata fedha za miradi ya maendeleo na huduma za kijamii.
Mwisho