Home LOCAL MBUNGE BONAH AFURAHISHWA NA UTEKLEZAJI WA MIRAD SEGEREA

MBUNGE BONAH AFURAHISHWA NA UTEKLEZAJI WA MIRAD SEGEREA

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli akiwa na Mwenyejiti wa Serikali ya Mtaa Mivinjeni Buguruni Fadiga Legele leo Julai 19/2021 katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya Jimbo la Segerea (PICHA NA HERI SHAABAN)

 

Msimamizi wa Mradi wa kituo cha Daladala Kinyerezi akizungumza na Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli leo Julai 19/2021 katika ziara ya Jimbo kugagua miradi hiyo (kulia wa pili )Diwani wa Kinyerezi Leah Ng’itu na Mhandisi wa TARURA Wilaya ya Ilala (PICHA NA HERI SHAABAN)

Makatibu waJimbo la Segerea wakiwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli na Diwani wa Kinyerezi Leah Ng’itu leo Julai 19/2021 wakati wa ziara ya Jimbo hilo kuangalia miradi ya maendeleo ziara iliyoandaliwa na Mbunge Bonah (PICHA NA HERI SHAABAN).

Diwani wa kata ya Buguruni Busoro Pazi akizungumza Jambo na Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli leo Julai 19/2021 Mbunge wa Jimbo la Segerea amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo (PICHA NA HERI SHAABAN)

Na: Heri Shaaban, DAR ES SALAAM.

MBUNGE wa jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli amelizishwa na utekekezaji wa Miradi ya maendeleo jimbo la Segerea Wilayani Ilala .

Mbunge Bonah aliyasema hayo Dar es Salaam jana  katika ziara yake ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo ipo jimboni humo.

Akizungumza katika ziara hiyo ya kutembelea kata ya Kinyerezi,Tabata na Buguruni na Makatibu wa Jimbo alisema dhumuni la ziara hiyo kuangalia utekelezaji wa miradi ya serikali ambayo inajengwa na mingine hipo hatua za mwisho

“Nimeanza ziara endelevu katika jimbo la Segerea ya kutatua kero na kuangalia utekelezaji wa miradi ya serikali ambayo inajengwa naomba wananchi wa Segerea mtunze miradi yenu ” alisema Bonah.

Bonah alimpongeza Rais Samia Hassan Suluhu  kwa kifanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa jimboni humo    ikiwemo miradi ya DMDP  kituo cha Daladala Kinyerezi, na Barabara ya Gongolamboto yenye thamani ya shilingi bilioni. 17 .

Katika ziara hiyo Bonnah pia amepata nafasi ya kuzungumza na wananchi mbalimbali ambapo katika Mtaa wa Kifuru Kata ya Kinyerezi wameomba ujenzi wa barabara ya NST Bangulo uharakishwe kwani wamekuwa wakipata adha kubwa hasa wakati wa mvua.

Injinia Mahobe Abdul akimweleza mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli, maendeleo ya ujenzi wa stendi hiyo.

Naye Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Leah Ng’itu, ameomba wasaidiwe barabara za ndani kwa kuweka vifusi pamoja na kukarabati maeneo korofi kwenye barabara za lami.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buguruni, Busoro Pazi, amesema ujenzi wa mfereji katika Mtaa wa Mvinjeni utakuwa ni suluhisho la kero ya mafuriko katika eneo hilo.

“Tunamshukuru mbunge wetu kwa juhudi kubwa alizozifanya kuhakikisha katika Mtaa wa Mivinjeni mfereji huu unajengwa, changamoto ya maji kutoka katika Mto Msimbazi kwenda kwenye makazi ya wananchi ilikuwa ni kubwa sana lakini kupitia ujenzi wa mfereji kero hii itaisha kabisa,” alisema  Pazi.

Diwani Busoro Pazi aliwataka  Wananchi kulipa kodi kila wakati ili Serikali iweze kupata fedha za miradi ya maendeleo na huduma za kijamii.

Mwisho

Previous articleWAZIRI BITEKO ATAKA MGODI KULIPA FEDHA ZA KIJIJI NDANI YA SIKU 60 MARA.
Next articleKAHAMA YAZINDUA MAONYESHO MAKUBWA YA KIMATAIFA YA UWKEZAJI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here