Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa (wa kwanza kushoto) akitoa maelezo mbele ya Mgeni rasmi Mhandisi Zenna Ahmed Said (wa pili kushoto mwenye koti nyekundu) alipotembelea Banda la TCU kupata maelezo ya namna Tume hiyo inavyotekeleza Majukumu yake. (kulia) ni Afisa Mwandamizi wa Udhibiti Ubora TCU
Afisa Udhibiti Ubora Mwandamizi wa TCU Hilda Kawiche (kushoto) akimueleza Mgeni rasmi Mhandisi Zenna Ahmed Said namna ambavyo Tume hiyo inatekeleza Majukumu yake ya kudhibiti ubora wa Viwango vya Elimu inayotolewa na Vyuo Vikuu mbalimbali hapa nchini.
|
Picha ya Pamoja ya Watumishi wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) wakiwa kwenye Banda lao katika siku maalum ya ufunguzi wa Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyofunguliwa rasmi leo Julai 27,2021 Jijini Dar es Salaam.
|
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanziber Mhandisi Zenna Ahmed Said akihutubia wakati akifungua rasmi Maonesho hayo leo Julai 27,2021 katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es Salaa.
Katibu Mtendaji wa TCU Prof. Charles Kihampa akitoa hotuba yake ya utangulizi kwenye halfa fupi ya ufunguzi wa Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na TCU Jijini Dar es Salaam.
Makamu mMwenyekiti wa TCU na Makamu Mkuu wa Chuo cha kumbukumbu ya Hurbert Kairuki Prrof. Charles Mgone akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kwenye Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es Salaam.
Prof. Charles Kihampa Katibu Mtendaji wa TCU (Kushoto) akiwa na Mgeni rasmi Mhandisi Zenna Saidi Katibu wa Baraza la wawakilishi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mara baada ya Mgeni huyo kuwasili viwanjani hapo na kuanza kutembelea Mabanda ya washiriki wa Maonesho hayo Jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Saidi leo Julai 27,2021 amefungua rasmi Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU).
Maonesho hayo ya siku sita yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam yameshirikisha Taasisi mbalimbali za Elimu ya Juu nchini ambapo katibu Mkuu huyo alipata nafasi ya kutembelea mabanda ya washiriki hao na kujionea shughuli mbalimbali ikiwemo ya udahili wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza papo hapo.
Akizungumza wakati akihutubia kwenye hafla fupi ya ufunguzi Mhandisi Zena amezitaka Taasisi hizo na Vyuo Vikuu kote nchini kusimamia weledi wa waombaji ili kuweza kupata wanafunzi wenye sifa stahiki watakaoweza kulisaidia Taifa na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa TCU Profesa Charles Mgone amesema kuwa Tume hiyo imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuhakikisha Elimu inayopatikana kwenye Vyuo na Taasisi za Elimu ya Juu inakidhi viwango na ubora.
Awali akitoa hotuba yake ya ukaribisho Karibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Profesa Charles Kihampa amesema kuwa maonesho hayo yatafanyika viwanjani hapo kwa siku sita nakwamba Taasisi zote zilizopo kwenye Maonesho hayo zimejiandaa vema kuweza kuwahudumia wananchi na wadau wote wa Elimu kwa ujumla ikiwemo kufanya udahili ndani ya mabanda yao.