Home BUSINESS KAHAMA YAZINDUA MAONYESHO MAKUBWA YA KIMATAIFA YA UWKEZAJI

KAHAMA YAZINDUA MAONYESHO MAKUBWA YA KIMATAIFA YA UWKEZAJI

 

Na: Saimon Mghendi,KAHAMA.

Wilaya ya Kahama imeandaa maonyesho makubwa ya uwekezji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo madini,kilimo,biashara,elimu Pamoja na mambo mengine, Maonyesho yanayotarajiwa kuanza July 30 na kumalizika ifikapo august 8 ambapo yanatarajiwa kuhudhuriwa na wafanyabiashara Pamoja na wajasiriamali wapatao 450 kutoka ndani na nje ya nchi.

Akifafanua katika kikao na waandishi wa Habari kilicho fanyika katika ofisi yake leo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, amesema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi kilichoopo katika manispaa ya Kahama, wameandaa maonyesho hayo kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara na wajasiriamali Pamoja na wateja wao.

Aidha Kiswaga amesema kuwa maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja vya  Kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi, na kuwataka wafanyabioashara Pamoja na wajasiriamali wote waliopo ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa hiyo.

Kwa upande wake Mratibu wa Maonyesho hayo ambae pia ni Afisa masoko kutoka kampuni ya GS1 Tanzania, Shabani Mikongoti, amesema kuwa wameandaa maonyesho makubwa ambayo ayajawahi kutokea katika kanda ya ziwa ambapo maonyesho hayo yatafanyika kwa saa 24 tofauti na maonyesho mengine na yatakua na vivutio mbalimbali ikiwemo Wanyama pori.

Maonyesho ya Kahama Investment Trade Fair yanayotarajiwa kuanza July 30 na kumalizika august 8 yamebeba kauli mbiu isemayo “KAHAMA NI KITOVU CHA BIASHARA UKANDA WA MAZIWA MAKUU”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here