Home LOCAL ILALA YAANZA KUATOA ELIMU YA UVIKO-19 NDANI YA DALADALA

ILALA YAANZA KUATOA ELIMU YA UVIKO-19 NDANI YA DALADALA

Afisa Mtendaji wa Kata ya Liwiti Wilaya ya Ilala IGINAS MAEMBE Leo Julai 29 /2021 ameanza kutekeleza agizo LA Serikali kutoa elimu katika Daladala za Segerea na kugawa Barakoa kwa abiria ambaye ajavaa Barakoa hizo za kujikinga na COVID (PICHA NA HERI SHAABAN)
Na: HERI SHAABAN.

AFISA Mtendaji wa Kata ya Kiwiti Iginas Maembe Leo ameazindua Kampeni endelevu ya utoaji wa Elimu ya Kujikinga na ugonjwa wa Mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO-19 ndani ya daladala zinazofanya safari zake Barabara ya Segerea  zinazosimama  Liwiti .
Katika utoaji wa elimu sambamba na utoaji wa  barakoa kwa abiria ambao hawana Barakoa ambapo daladala ikifika  Liwiti wanapewa elimu na kukabidhiwa barakoa moja bure

“Liwiti tumepokea agizo la Serikali la uvaaji Barakoa na katika Kata yangu nakagua Daladala zote kutoa elimu na abiria ambaye ajavaa barakoa anapewa bure ili aweze kujikinga na mambukizi ya CORONA “ alisema Iginas

Aidha alisema ametumia fursa hiyo kutoa elimu ya ugonjwa wa UVIKO-19 katika Kata hiyo kwa nafasi yake   Kiongozi Kata wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Liwiti 

Iginas aliwataka wananchi kusikiliza maelekezo ya Serikali pamoja  na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pindi wanapotoa Elimu ya kujikinga wachukue hatua mbalimbali  .

Katika utoaji wa elimu hiyo aliongozana na Watoa huduma ngazi ya Jamii ambao wapo chini ya Ofisi ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji  pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here