Home LOCAL NI LAZIMA TUKAPIGANIE BUNGENI BARABARA ZA VIJIJINI ZIJENGWE-MAKAMBA

NI LAZIMA TUKAPIGANIE BUNGENI BARABARA ZA VIJIJINI ZIJENGWE-MAKAMBA

Na Mwandishi Wetu, Lushoto | Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba ameahidi Kuendelea kulipigania na kulipeleka Bungeni suala zima la Changamoto ya barabara lilopo maeneo ya vijijini ili kuwepo usawa kati ya mjini na vijijini.

Hayo ameyasema leo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mponde kuhusu Serikali ya awamu ya sita ilivowapatia sh. 1.5 9 bilion kwa ajili ya kujenga Barabara kwa kiwango cha lami na changarawe kwenye baadhi ya Barabara zilizopo kwenye Jimbo hilo.

Makamba alitaja barabara zitakazonufaika na fedha hizo kwa kujengwa kwa kiwango cha changarawe kuwa ni Barabara ya Mgwashi – Mbelei yenye urefu wa kilometa 23.8 ,Bumbuli -Mayo, Vulii- Mahezangulu hadi Magoma kilometa 15.4,Vuga – Mponde hadi Wena kilometa 21.2 na Balangai – Tamota na Vuliii yenye urefu wa kilometa 13.4,Soni -Mponde kilometa 13.4 pamoja na Bumbuli center itakayojengwa kwa kiwango cha lami.

Mbunge huyo alisema sio sawa kuona mjini wanajengewa barabara za juu na zinapanuliwa kila kukicha lakini vijijini ambako wapiga kura wengi wapo, wanapata shida kupitisha mazao yao kutokana na barabara kuwa changamoto hasa wakati wa msimu wa mvua.

Inauma mtu analima chai yake anapalilia mwenyewe lakini anashindwa kupeleka kiwandani sababu barabara inautelezi hii sio sawa kabisa” alisema Makamba.

Mimi huwa nawaambia wenzangu kama kweli tunaweka barabara za maghorofa hatushindwi kuwasaidia watu wa vijijini kwani wanachotaka barabara zao zipitike wakati wote hasa kipindi cha mvua” Alisema Makamba

Alisisitiza kuwa lazima kuwepo na haki sawa katika kupeleka maendeleo ya nchi ,haiwezekani kwa Dar es Salamu tu kuna barabara moja ina njia nne mpaka sita ambapo alitolea mfano yaani barabara moja ni kama kiwanja cha mpira yaani barabara inakuwa kwenye kona ile na kona nyingine.

Aidha alieleza kuwa moja ya malengo makubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kupambana na barabara za vijijini.

Aliongeza kwamba serikali imepanga ifikapo mwaka 2025 Watanzania wanaokipigia chama cha Mapinduzi kila mwaka angalau barabara zao ziwe zinapitika wakati wote sababu hao tunaowajengea za magorofa yawezekana baadhi yao hawapigi ata kura wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo alisema yeye kama Mbunge kiu yake ni kuona wananchi wake wanaondokana na changamoto hiyo ambayo ni kero kubwa ukilinganisha na jiografia ya maeneo ya Jimbo la Bumbuli

Makamba ameanza rasmi ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi katika Jimbo lake.

Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akikagua Maabara ya sayansi katika shule ya sekondari ya kiviricha kata ya Usambara iliopo Halmshauri ya Bumbuli Mkoani Tanga ambayo zahanati hiyo Mbunge ameichangia mil.10,Wananchi milion 25 na serikali kuu Milion 35.
Previous articleILALA YAANZA KUATOA ELIMU YA UVIKO-19 NDANI YA DALADALA
Next article“MARUFUKU KWA HOSPITALI ZA UMMA NA BINAFSI KULIPISHA WANANCHI GHARAMA ZA CHANJO”- SERIKALI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here