Home LOCAL ANNA MGHWIRA AFARIKI DUNIA

ANNA MGHWIRA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia leo Alhamisi Julai 22, 2021 katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mdogo wa Anna Mghwira na marafiki zake wa karibu wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho leo.

“Ni kweli Mghwira amefariki mchana huu, alikuwa amezidiwa akawa amepelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU),” amesema mdogo wake.

Zaidi ya wiki moja iliyopita alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua ambapo baadaye hali yake kuwa mbaya alihamishiwa hospitali ya Mount Meru.

CHANZO:MWANANCHI

Previous articleTANGAZO MAALUM KUTOKA TCRA.
Next articleRAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MAMA MGHWIRA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here