Home BUSINESS WATANZANIA MSINUNUE BIDHAA BILA KUHAKIKI ALAMA YA UBORA YA TBS: DKT. NGENYA

WATANZANIA MSINUNUE BIDHAA BILA KUHAKIKI ALAMA YA UBORA YA TBS: DKT. NGENYA

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  Dkt Yusuph Ngenya akizungumza na waandishi wa habari

NA: OSCAR ASSENGA, TANGA.

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  Dkt Yusuph Ngenya ametoa wito kwa  watanzania wasinunue bidhaa yoyote bila kuhakikisha kwamba ina alama ya ubora kwa bidhaa zinazozalishwa nchini.

Ngenya aliyasema hayo eneo la Mwahako Jijini Tanga  kunakoendelea maonesho ya nane ya Biashara ambapo alisema hatua hiyo itasaidia kuwaondolea hasara ambazo wamekuwa wakikumbana nazo kutokana na bidhaa wanazonunua kutokuwa na ubora unaotakiwa.

Alisema kwani bidhaa zimekuwa na athari nyingi katika matumizi ya binadamu hiyo ni muhimu watanzania kutambua kwamba wanaponunua  bidhaa wanapaswa kuzikagua na kuona kama zina ubora unaotakiwa ili kuweza kuepukana na majanga ambayo yanaweza kuwakuta kutokana na bidhaa  feki.

“Lakini hata katika operesheni zetu ambazo tumekuwa  tukizifanya tunagundua  bidhaa gani ambazo zinaingizwa kwenye masoko na hazina ubora ikiwemo bidhaa za ujenzi vifaa vya umeme vingi vinakuja feki hivyo tujitahidi kuvitambua na kuviondoa  kwenye soko kwani mfano vifaa vya umeme madhara yake vinaweza kushika moto na kuweza kuharibu mali”Alisema Mkurugenzi huyo wa TBS.

Akizungumzia lengo la uwepo wao kwenye maonyesho hayo ya nane ya biashara alisema wapo kwa ajili ya kuwaelimisha wananchi kuhusu shughuli za TBS na namna ya kupata huduma zao.

“TBS pamoja na mambo megine kwenye maonyesho kama haya  tunawakaribishaw kuweza kuwaelimisha kwa mfano wale wanaotaka kupata huduma za TBS ikiwemo  bidhaa zao ziweze kupata alama ya ubora lakini pia tunashughulikia uuzaji wa bidhaa za chakula na vipodozi kuweza kupata usajili wa shughuli zao”Alisema Mkurugenzi huyo mkuu wa

TBS.

Hata hivyo aliwataka wajasiriamali watengenezaji  wa bidhaa ndogo ndogo ni rahisi kwanza kwenda SIDO kupata mafunzo ambayo yatawasaidia kupata cheti kitachowawezesha kupata barua kutoka SIDO na baadae waende   TBS kuweza kutambulika na wao watafanya kazi iliyobakia mpaka kuhakikisha bidhaa yao inapata ubora.

Previous articleMAJALIWA: TUMIENI NISHATI MBADALA
Next articleRAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA MWENDOKASI YA MBAGALA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here