Home LOCAL RC ATOA WIKI MBILI KWA MANISPAA YA TABORA KUSAFISHA NA KUKARABATI MACHINJIO...

RC ATOA WIKI MBILI KWA MANISPAA YA TABORA KUSAFISHA NA KUKARABATI MACHINJIO YA KARIKOO

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kushoto) akitoa jana maagizo kwa viongozi wa Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kutembelea machinjio ya Karikoo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (katikati) akikagua leo maeneo mbalimbali ya machinjio ya Karikoo yaliyopo Manispaa ya Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kulia) akiangalia  leo jinsi sakafu ya machinjio ya Karikoo yaliyopo Manispaa ya Tabora ilivyoharibika na kuruhusu damu na maji machafu kutuwama.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (wa pili kutoka kulia) akiangalia jinsi zoezi la ukaushaji wa ngozi unavofanyika katika machinjio ya Karikoo wakati wa ziara leo ya siku mmoja ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika.


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kushoto) akisalimia leo na viongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) na viongozi wa Wilaya ya Tabora alipowasali kwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora kwa ajili ya ziara ya kutembelea machinjio ya Karikoo.

 

NA: TIGANYA VINCENT,RS TABORA.

MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ametoa wiki mbili kwa uongozi wa Manispaa ya Tabora kukarabati na kusafisha Machinjio ya ng’ombe ya Karikoo ili kuweka mazingira mazuri ya utoaji wa huduma.

Alisema hali ya usafi katika eneo hilo hauridhishi na kuongeza ndani ya kipindi hicho uchafu wote yakiwemo maji yanatokana na usafishaji nyama ndani ya Machinjio yaelekezwe sehemu stahili.

Balozi Dkt. Batilda alitoa kauli hiyo leo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kukagua machijio ya Karikoo ambayo ndio yanatoa huduma ya uchinjaji wa ng’ombe , mbuzi na kondoo kwa ajili ya mboga za wakazi wa Manispaa ya Tabora na maeneo ya jirani.

Alisema Manispaa ya Tabora wahakikishe wanaweka malumalu (tiles) kwenye sakafu na kupiga rangi wakati wakisubiri kujenga mradi mkubwa wa kimkati wa machijio ya kisasa.

Balozi Dkt. Batilda alisema sanjari na hilo ni vema wakaboresha ukaushaji wa ngozi ili kuziongezea thamani kuliko ilivyo hivi sasa ambapo zinawekwa kwenye udongo wakati wa ukaushaji.

Aidha alisema uboreshaji wa machinjio hayo utasaidia kutoa huduma nzuri kwa wateja na mapato ya Halmashauri yataongeza kutokana na tozo wanatoza.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Ismail Nawanda alisema watajitahidi kutumia fedha za ndani kukarabati maeneo yote yaliyochakaa na kufanya usafi.

Alisema ndani ya wiki mbili watakamilisha taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kuhusu maendeleo ya zoezi hilo.

Awali Mkurugenzi Mtendaji Bosco Ndunguru alisema machinjio hiyo inaweza wa kuchinja ngo’ombe 80 kwa siku.

Previous articleYACOUBA SONGNE AIPELEKA YANGA SC FAINAL KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION (FA).
Next articleRAIS SAMIA AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI TANZANIA (TEC)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here