Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa, akiwasilisha mada na kutoa ufafanuzi kuhusu utendaji wa BRELA kwa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda Biashara na Mazingira, mapema Juni 9, 2021 jijini Dodoma. Kamati hiyo imeipongeza BRELA kwa kwa kuboresha utendaji kazi, kwani kwa sasa huduma za usajili wa biashara na leseni zinafanyika kwa njia ya mtandao.