Home LOCAL NATAKA MJI WA KAHAMA UWE MJI WA KISTAREHE – DC KISWAGA

NATAKA MJI WA KAHAMA UWE MJI WA KISTAREHE – DC KISWAGA

NA: SAIMON MGHENDI, KAHAMA

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswga Amesema kuwa ukitaka watu wafanye Kazi kwa bidi uwaekee starehe kwani kati ya vitu ambavyo vinaumiza sana Duniani ni mawazo (Stress) hivyo tunataka tupunguze stress na kuongeza happiness.

Kiswaga ameyasema hayo leo wakati akijitambulisha kwa watumishi wa serekali ya wilaya ya Kahama, pamoja na madiwani kataka ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya kahama, mara baada ya kuapishwa kuwa mkuu mpya wa Wilaya hiyo.

“Kwahiyo tutafanya biashara masaa 24 kwnye mji huu, naomba wenzetu wa mabenki mtusaidie surveillance camera ambazo tutazifunga kwenye mitaa hiyo, mitaa hiyo itakua maeneo  salama kama uko Uswizi, hiyo ndo Kahama ya picha  tunayoitaka”, Alisema Kiswaga.  

Aidha Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa anataka kuugeuza mji wa kahama kuwa mji wakibiashara japokua watu wanasema ni mji wa Madini na kuongeza kuwa anataka mji wa kahama uwe kinara wa madini,biashara pamoja na kilimo.

Vile vile Kiswaga amewashawishi wananchi wa kahama kuzaa Watoto kwa wingi ili idadi ya watu iongezeke, jambo litakalo pelekea kupata raslimali watu, huku akitolea mfano wa mataifa makubwa ya ulaya pamoja na nchi ya China walivyoendelea kwa kuwa wana watu wengi zaidi.

Previous articleSERIKALI KUJENGA KIWANDA CHA KUZALISHA DAWA NCHINI.
Next articleKUTOKA BUNGENI JIJINI DODOMA MCHANGO WA MHE, DEO MWANYIKA MBUNGE WA JIMBO LA NJOMBE MJINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here