Home LOCAL MUFTI ZUBERI AWATAKA WATANZANIA WASICHAFUE HALI YA HEWA

MUFTI ZUBERI AWATAKA WATANZANIA WASICHAFUE HALI YA HEWA

 

Mufti wa Tanzania Abubakari Zuberi akiongea jambo na Shekhe wa Mkoa wa Dar es salam Alhad Mussa Salum ,katika kongamano la kiislam lililoandaliwa na Baraza la Kiislam Tanzania BAKWATA kwa kushirikiana na Kituo cha Kiislam cha Misri Dar es salam Jana (PICHA NA HERI SHAABAN)

Mufti wa Tanzania Abubakari Zuberi akiwasalimia mashekhe wa   Mkoa wa Dar es salam katika kongamano la kiislam lililoandaliwa na Baraza la Kiislam Tanzania BAKWATA kwa kushirikiana na Kituo cha Kiislam cha Misri Dar es salam Jana(katikati)Shekhe wa mkoa Alhad Mussa Salum (PICHA NA HERI SHAABAN)

Baadhi ya mashekhe wa Mkoa wa Dar es salam wakiwa katika kongamano la Dini ya Kiislam, lililoandaliwa na Baraza la Kiislam Tanzania Bakwata na Kituo cha Kiislam cha Misri(PICHA NA HERI SHAABAN).

Na: Heri Shaaban, DAR ES SALAAM.

MUFTI wa Tanzania Shekhe  Abubakar Zuberi amewataka Watanzania kudumisha amani na mshikamano wasichafue hali ya hewa katika nchi yetu.

Shekhe Abubakari Zuberi aliyasema hayo Dar es Salaam leo katika Kongamano la dini ya Kiislam lililoandaliwa na Baraza Kuu la kiislam Tanzania BAKWATA kwa kushirikiana na Kituo cha Kiislam cha Misri.

Akizungumza katika kongamano hilo Mufti alisema tunajivunia amani iliyopo katika nchi yetu Tanzania hivyo tudumishe amani iliyopo kwa umoja wetu tusikubali hali ya hewa kuchafuliwa.

“Amani ndio jambo la msingi sana nawaomba Watanzania tudumishe umoja na mshikamano wetu tuzidi kuchapa kazi katika kuisaidia Serikali yetu na kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu” alisema Mufti.

Mufti alisema amani iliyopo hapa nchini ni lulu tuendelee kudumisha mshikamano  na kujenga uzalendo kwa ajili ya nchi yetu.

Kwa upande wake Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum alisema Uislam kuchafuliwa sio vizuri kila moja anaitaji amani ,Wanyama na ndege pia wanaitaji amani  wakikosa usalama unapomfuata ndege au Kunguru anaruka .

Shekhe Alhad alisema ,Waislam na Afrika wanaendelea kuombea amani katika nchi yetu na Afrika kwa ujumla huku wakijenga mausihano mazuri .

Aidha alisema katika nchi yetu kuna mausihano mazuri dini zote na wanaendelea kushirikiana pamoja wote marafiki baina ya dini hizo.

Mkurugenzi wa Kituo cha Kiislam Misri Tanzania Shekhe Jamal Abdulmdaty alisema 

Mafunzo hayo ya dini  inatufunza uislam dini ya kweli na umoja tusaidiane katika wema na wale si waislam pia wasaidiane  mtu atakaye muua mwezake awezi kuona pepo.

Mwisho

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.MOSI JUNI 19-2021
Next articleDKT.GWAJIMA AKUTANA NA WATUMISHI WA WIZARA YAKE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here