Home BUSINESS MTENDAJI KATA YA CHELA AWAPONGEZA WACHIMBAJI WADOGO

MTENDAJI KATA YA CHELA AWAPONGEZA WACHIMBAJI WADOGO

Na: Cymon Mgendi, KAHAMA. 

Afisa Mtendaji wa Kata ya Chela Ilyopo Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga  Evagisla John Amesema kuwa kuwepo kwa machimbo ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika kata hiyo kuna mchango mkubwa katika jamii inayozunguka eneo hilo ambapo wachimbaji hao wamekua wakishiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kukarabati shule pamoja na kutoa mchango kwa jamii hiyo pale wanapo itajika kufanya hivyo.

Afisa mtendaji huyo ameyasema hayo leo wakati akiwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya miradi iliyotekelezwa na wachimbaji wadogo katika kata hiyo na kuongeza kuwa wachimbaji hao wamekua wakipunguza mzigo kwa kwa  serekali pamoja na wananchi wa maeneo hayo

Aidha Evagisla John anatumia fursa hiyo kuiomba serekali pamoja na taasisi za kifedha kuwawezesha wachimbaji hao kwa kuwapa mikopo yenye riba nafuu iliwaweze kuonmdokana na dhana duni ili waweze kuchimba kisasa na kupata mapato zaidi.

Kwa upande wake meneja Mgodi wa Kasi mpya Cosmas Erick Amesema kuwa wamekua wakiipa ushirikiano serekali  pamoja na kushirikiana na jamii inayozunguka eneo hilo na kuongeza kuwa kilio kikubwa cha wachimbaji wa eneo hilo ni serekali kuwapelekea huduma ya umeme ili waweze kuchimba kwa ufanisi pamoja na kupunguza gharama.

Nae Katibu wa Mbunge wa jimbo la msalala Edisoni Erasto amesema kuwa mbunge wa jimbo hilo Idi kassim Idi anawapongeza wachimbaji wadogo kwa kujitoa katika maendeleo ya jamii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here