Home LOCAL MEYA KUMBIMOTO NA DIWANI SULTAN WAWEKEZA SEKTA ELIMU

MEYA KUMBIMOTO NA DIWANI SULTAN WAWEKEZA SEKTA ELIMU

 

Meya wa Halmashauri ya Jiii la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akitoka kukagua eneo la ujenzi wa shule ya Msingi Olimpio Leo Juni 21/2021  katika shule hiyo wamechanga Jumla ya shilingi mililioni  100,900,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya ghorofa 4(katikati)Diwani wa Upanga Mashariki Sultan Salim na Naibu Meya wa Halmashauri ya jiji Saddy Kimji (PICHA NA HERI SHAABAN)

Shekhe wa Wilaya ya Ilala Adam Mwinyipingu (kulia)akiongoza Dua Maalum  leo Juni 21/2021 kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa vyumba vys madarasa ya Shule ya Msingi Olimpio ghorofa NNE (kushoto)Meya wa Halmashauri ya Jiji LA Dar es Salaam Omary Kumbilamoto Naibu Meya wa Halmashauri hiyo Saady Kimji na Diwani wa Upanga Mashariki Sultan Salim (PICHA NA HERI SHAABAN)

Na: HERI SHAABAN, DAR ES SALAAM.

MEYA wa halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto Diwani Sultan Salim , wawekeza katika sekta ya Elimu kwa kuanza na Dua Maalum kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Olimpio.

Dua Maalum ya ujenzi wa ghorofa NNE ya shule ya Msingi Olimpio iliongozwa Jana  Juni 21/2021 na Shekhe wa Wilaya ya Ilala  Adam  Mwinyipingu shuleni hapo.

Akisoma Dua hiyo shekhe wa Wilaya Adam Mwinyipingu aliomba kwa mwenyezi Mungu mafundi  awafanyie wepesi ujenzi usimame kwa wakati ili watoto waweze kusoma .

Pia shekhe wa Wilaya aliomba kamati ya Shule na wasimamizi kusimamia ujenzi huo.

Kwa upande wake Meya wa halmashauri ya jiji Omary Kumbilamoto aliipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri matokeo ya mwaka 2020 ya elimu ya msingi .

Meya Kumbilamoto alipongeza Kamati ya shule hiyo Diwani wa Upanga Mashariki   Sultan Salim ,Mkurugenzi wa Jiji ,Mkuu wa Wilaya ya Ilala na Katibu Tawala    kwa kuwasimamia Wazazi wa Shule hiyo vizuri na kufanikisha kujenga ghorofa NNE katika shule hiyo.

Meya Kumbilamoto alisema wanaunga  mkono juhudi za serikali katika sekta ya elimu kuakikisha watoto wote wanapata elimu.

Alisema Taifa lolote ili liweze kuendelea na kupata maendeleo lazima wananchi wake wasome.

Alisema halmashauri hiyo inatekeleza agizo la Serikali mpango  wa elimu bure kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari.

Diwani wa Upanga Mashariki Sultan Salim alisema anasimamia katika sekta ya elimu kuakikisha ndani ya Kata hiyo elimu inakuwa  na watoto wote wanasoma.

Pia Diwani Sultan Salim alisema vipaumbele vyake vingine katika kata hiyo kuisaidia Serikali katika suala zima la ukusanyaji mapato  ili Serikali ifikie malengo yake kuendeleza miradi ya maendeleo.

Mwisho

Previous articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO J.NNE JUNI 22-2021
Next articleLHRC YALAANI TUKIO LA KUCHOMWA MOTO MTOTO WA KIKE WA MIAKA MINNE.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here