Home LOCAL LENGO LA JUMUIYA YA KIISLAM YA AHMADIYYA NI KUWAFANYA WATU WAISHI KATIKA...

LENGO LA JUMUIYA YA KIISLAM YA AHMADIYYA NI KUWAFANYA WATU WAISHI KATIKA NJIA YA KUMPENDEZA MUNGU NA SIO SIASA AMA UGAIDI

Abdul Rahman Mohammed Ame, Katibu mkuu wa Jumuhiya hiyo, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habari na pembeni ni Amir na Mbashiri Mkuu Jumuiya ya Kiislam ya AHMADIYYA, Tahir Mahmood Chaudhry.

Amir na Mbashiri Mkuu Jumuiya ya Kiislam ya AHMADIYYA, Tahir Mahmood Chaudhry akiongoza ibada.
Na, Saimon Mghendi: Kahama.

Lengo kubwa la Jumuiya ya Kiislam ya AHMADIYYA ni kuwafanya watu waishi katika njia impendezayo mwenyezi Mungu pamoja na Mtume wake Muhammad (S.A.W), sambamba na kutoa elimu juu ya watu wanaofanya maovu ya kuua vikongwe pamoja na watu wenye ualbino na kamwe Jumuiya hiyo hainampango wa kujiingiza katika siasa, biashara, ugaidi au jambo lolote litakalo enda kinyume na serekali.

Hayo yamesemwa na Amir na Mbashiri mkuu wa jumuiya hiyo jana, Tahir Mahmood Chaudhry , katika Hitimisho la Kongamano la siku Mbili la Jalsa Salana, liliofanyika katika Manispaa ya Kahama Ambapo ndiyo Makao makuu ya Jumuiya hiyo kwa Mkoa wa Shinyanga.

Hata Hivyo Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Kiislam ya AHMADIYYA, Tahir Mahmood Chaudhry, Amesema kuwa Jumuhiya imekua na ushirikiano mzuri na Serekali pamoja na wanachi, ambapo imekua ikifadhili kwa kuchimba visima zaidi ya 150 bure kwa Kwa mkoa wa Shinyanga, ilikuwezesha jamii husika kupata huduma muhimu ya maji.

Waumini wa Jumiya hiyo kutoka sehemu mbali mbali wakati wa kongamano hilo

Previous articleSERIKALI YAJIPANGA KUKOMESHA UKATILI WA KIJINSIA NDANI NA NJE. YA VYOMBO VYA HABARI
Next articleRAIS SAMIA ASHIRIKI KIKAO CHA SADC MJINI MAPUTO, MSUMBIJI, AREJEA NCHINI, JIJINI DODOMA, LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here