Home LOCAL KENANI KIHONGOSI ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA VIJANA WA CCM...

KENANI KIHONGOSI ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM)

Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM, Kenani Kihongosi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka akizungumza na vyombo vya habari Makao Makuu ya CCM, Jijini Dodoma leo ambapo pamoja na mambo mengine alielezea uamuzi wa Kamati Kauu ya Halmashauri Kuu ya CCM, kumteua Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Keneni Kihongosi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM.
Shaka akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

 DODOMA.

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Kenani Kihongosi  kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM.


Kihongosi anachukua nafasi ya Raymond Mwangwala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro.


Uteuzi huo umetangazwa  mbele ya vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Shaka Hamdu Shaka katika Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma mara baada ya kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete kumalizika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here