Home LOCAL JESHI LA POLISI LA WAONYA MADEREVA WA MABASI YA ABIRIA

JESHI LA POLISI LA WAONYA MADEREVA WA MABASI YA ABIRIA

Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Wilboard Mutafungwa, Akizungumza na madereva.

Na, Saimon Mghend, KAHAMAi l

Jeshi la polisi limefanya ukaguzi wa mabasi pamoja na kutoa Elimu kwa madereva wa mabasi  yaendayo mikoani na nchi jirani katika kituo kikuu cha mabasi cha Manispaa ya Kahama.

Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Wilboard Mutafungwa, Akizungumza na madereva hao mapema leo kabla ya kuanza safari amewataka kuzingatia sheria za usalama barabrani ili kujiepusha na ajali zisizo za lazima.

Hataivyo Kamanda Mutafungwa Amesema Jishi la polisi nchini limekwisha kuwafungia leseni za udereva, Madereva wa mabasi 27 kwa makosa kadhaa ikiwemo ya mwendo kasi kwa kipindi cha miezi sita, Nakutoa Onyo kali kwa madereva wengine ambao hawatazingatia sheria za usalama barabarani.

Pia Kamanda Mutafungwa aliwataka abiria kutokukaa kimya na badala yake  kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pale ambapo wataona dereva anavunja sheria za uisalama barabarani.

Previous articleMAGAZETI YA LEO J.MOSI JUNI 5-2021
Next articleVYUO VYA MAENDELEO YA JAMII UFUNDI NA UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA JAMII

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here