Home LOCAL JAMII JENGENI TABIA YA KUTUNZA MAZINGIRA KWA KUFANYA USIFI KILA SIKU: RC...

JAMII JENGENI TABIA YA KUTUNZA MAZINGIRA KWA KUFANYA USIFI KILA SIKU: RC MONGERA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela akizungumza  katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani yaliyofanyika katika halmashauri ya Meru.

Wanafunzi kitoka shule mbalimbali wakionesha mabango mbalimbali yenye jumbe za uhamasishaji wa utunzaji wa mazingira katika kilele cha siku ya mazingira duniani yaliyofanyika halmashauri ya Meru.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela ameitaka jamii kujenga tabia ya kutunza mazingira kwa kufanya usafi kila siku huku akiwataka wadau wa mazimgira na mifumo ya Serikali kushirikiana kuijengea jamii uwezo katika suala zima la mazingira.

Mongela aliyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani yaliyofanyika katika Halmashauri ya Meru kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali ambapo alisema kuwa ili waweze kufanikiwa katika utunzaji wa mazingira juhudi hizo zinapaswa kuwa za kila siku.

Alisema kuwa suala la utunzaji wa mazingira na usafi ni suala ambalo lazima mtu ajengewe kama tabia hivyo juhudi wanazozifanya za kuwashirikisha watoto na shule mbalimbali zitazaa matunda makubwa.

“Watoto hawa  wanakuwa mkiwajengea tabia hii ya kutuza na kufanya usafi wa mazingira kwa sasa zitazaa matunda na kuwa mchango mkubwa kwa mazingira nchini kwetu,”Alisema Mongela.

Kwa upande wake Afisa mazingira kutoka Baraza la Taifa la uhifadhi wa mazingira (NEMC) Francis  Nyamhanga Alisema kuwa wananchi wanapaswa kutambua kuwa mazingira yao ni maisha yao hivyo watumie nishati mbadala ili kulinda na kugeuza mfumo wa ikolojia katika hali yake ya asili.

Alisema kuwa jamii inapaswa kupanda miti, kufanya usafi wa mazingira, kutunza vyanzo vya maji huku wakizuia ukataji wa miti na kutotiririsha maji machafu kwenye mito kwani kila mmoja ana jukumu la kutunza mazingira.

Aidha alieleza kuwa NEMC watafanya kazi pamoja na wadau wa mazingira ili kuhakikisha kuwa elimu ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira inawafikia watu wengi zaidi na kuhakikisha nishati mbadala inasambazwa na kuweza kuokoa misitu.

“Tunajukumu la kuhakikisha mazingira ya kanda yetu na nchi nzima kwa ujumla yanakuwa mazuri kwaajili ya sasa na vizazi vijavyo vikute mazingira yakiwa salama,” Alisisitiza Fransis.

Aidha akisoma ripoti ya mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru Afisa usafi na mazingira wa wilaya hiyo Charles Makama alisema kuwa changamoto iliyopo kwasasa ambayo inaleta madhara kwenye mfumo wa ikolojia ni pamoja na uchimbaji wa madini ya ujenzi katika eneo la ukanda wa juu ambapo ndipo kuna vyanzo vingi vya maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here