Home LOCAL DIWANI WA LIWITI KUZINDUA WIKI YA KERO KESHO JUNI 13

DIWANI WA LIWITI KUZINDUA WIKI YA KERO KESHO JUNI 13

 

Diwani wa kata ya Liwiti Alice Mwangomo akizungumza na wakazi wa Kata hiyo Juni 13/2021 katika kikao cha Serikali ya Mtaa kilichoandaliwa na Mwenyekiti Arafa Mshana kilichokuwa kinahusu Waraka wa Utekeleza maelekezo ya Serikali kuhusu ulinzi na Usalama ngazi ya kata na Mtaa (PICHA NA HERI SHAABAN)

Mkuu wa Polisi Tabata Mrakibu wa Polisi College Senkondo akizungumza na Wakazi wa Liwiti wakati wa kukabidhi Waraka wa utekelezaji maelekezo ya Serikali kuhusu Ulinzi na Usalama ngazi ya Kaya na Mtaa Waraka huo umetolewa na Afisa Mtendaji wa Liwiti Ignas Maembe (Katikati)kutoka kulia Mwenyekiti wa Mtaa Arafa Mshana na Diwani wa Liwiti Alice Mwangomo (PICHA NA HERI SHAABAN)

Afisa Mtendaji wa Kata ya Liwiti Ignas Maembe akisoma Waraka aliokabidhi kwa Wenyeviti wake wa Serikali za Mitaa Juni 12/2021 Waraka wa utekelezaji maelekezo ya Serikali kuhusu Ulinzi na Usalama ngazi ya Kaya na Mtaa ambapo Wapangaji wote wanatakiwa wajiandikishe katika daftati LA makazi (Katikati) Diwani wa Liwiti Alice Mwangomo na Mwenyekiti wa Liwiti Arafa Mshana (PICHA Na HERI SHAABAN)

NA: HERI SHAABAN, DAR ES SALAAM.

DIWANI wa kata ya Liwiti wilayani Ilala Alice Mwangomo kesho Jumatatu Juni 14 /2020 anazindua wiki ya  kusikiliza kero za Wananchi wake.

Uzinduzi huo wa kero Liwiti unatarajia kufanyika Ofisi za Kata Liwiti Wilayani Ilala Mkoani Dar es Salaam ambapo amewataka wakazi wa Kata hiyo kujitokeza kuwasilisha kero zao ambazo azijapata ufumbuzi wake..

Hayo yalisemwa Dar es Salaam Jana,katika mkutano wa adhara ulioandaliwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Liwiti Arafa Mshana uliokuwa ukijadili maswala ya ulinzi na usalama na maendeleo ya Mtaa huo.

“Nawaomba Wananchi wangu kesho ni siku maalum ya kuanza kusikiliza kero mjitokeze ofisi zetu za kata muwasilishe kero zenu kuanzia SAA mbili asubuhi hadi SAA kumi jioni” alisema Alice.

Akizungumzia maendeleo ya Kata ya Liwiti alisema  wanatarajia kujenga Sekondari ya Kata hiyo ambayo mikakati ya ujenzi imeanza  ujenzi wa gholofa ,na pesa zilizotengwa ni shilingi milioni  4 kwa sasa anatafutwa mkandarasi ujenzi huo uwanze eneo LA  Liwiti shule ya msingi.

Alimwagiza Afisa Mtendaji wa Kata hiyo kusimamia suala LA ujenzi tenda ikitangazwa vibarua wote wa kijenga ghorofa wawe wazawa wa Liwiti  sio watu wa nje.

Pia alisema amepokea milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Utawala za Walimu wa shule ya msingi Misewe ambapo ujenzi wake unatarajia kuanza Mara moja.

Amewataka wakazi wake kushirikiana katika kuleta maendeleo  ndani ya kata hiyo wakiwa na kero wawasilishe Mamlaka husika

Mwisho

Previous articleHABARI KUU ZILIZOTAWALA MAGAZETI YA LEO J.TATU JUNI 14-2021
Next articleUZINDUZI WA ALBAMU MBILI ZA MAMAJUSI ANGLIKANA MOSHI, ZAIDI YA MILIONI NANE ZAPATIKANA INJILI YAENEZWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here