NA: HERI SHAABAN, DAR ES SALAAM.
DIWANI wa kata ya Liwiti wilayani Ilala Alice Mwangomo kesho Jumatatu Juni 14 /2020 anazindua wiki ya kusikiliza kero za Wananchi wake.
Uzinduzi huo wa kero Liwiti unatarajia kufanyika Ofisi za Kata Liwiti Wilayani Ilala Mkoani Dar es Salaam ambapo amewataka wakazi wa Kata hiyo kujitokeza kuwasilisha kero zao ambazo azijapata ufumbuzi wake..
Hayo yalisemwa Dar es Salaam Jana,katika mkutano wa adhara ulioandaliwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Liwiti Arafa Mshana uliokuwa ukijadili maswala ya ulinzi na usalama na maendeleo ya Mtaa huo.
“Nawaomba Wananchi wangu kesho ni siku maalum ya kuanza kusikiliza kero mjitokeze ofisi zetu za kata muwasilishe kero zenu kuanzia SAA mbili asubuhi hadi SAA kumi jioni” alisema Alice.
Akizungumzia maendeleo ya Kata ya Liwiti alisema wanatarajia kujenga Sekondari ya Kata hiyo ambayo mikakati ya ujenzi imeanza ujenzi wa gholofa ,na pesa zilizotengwa ni shilingi milioni 4 kwa sasa anatafutwa mkandarasi ujenzi huo uwanze eneo LA Liwiti shule ya msingi.
Alimwagiza Afisa Mtendaji wa Kata hiyo kusimamia suala LA ujenzi tenda ikitangazwa vibarua wote wa kijenga ghorofa wawe wazawa wa Liwiti sio watu wa nje.
Pia alisema amepokea milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Utawala za Walimu wa shule ya msingi Misewe ambapo ujenzi wake unatarajia kuanza Mara moja.
Amewataka wakazi wake kushirikiana katika kuleta maendeleo ndani ya kata hiyo wakiwa na kero wawasilishe Mamlaka husika
Mwisho