Wananchi wa Minazi mirefu wakimsikiliza diwani Malisa katika mkutano wake wa kwanza wa hadhara Dar es Salaam Jana (PICHA NA HERI SHAABAN) |
NA: HERI SHAABAN.
DIWANI wa Kata ya Minazi Mirefu Godlisten Malisa amemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Hassan Suluhu maeneo ya wazi Hali ya hewa lilipo ndani ya kata hiyo ili litumike kwa ajili ya Shule na zahanati.
DIWANI Malisa alimwomba Rais jana katika mkutano wake wa kwanza wa kuwashuru wanachama na kueleza mikakati yake ya utekelezaji Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.
“Kata yetu imegawanywa katika Kata mama ya Kiwalani aina huduma za Jamiii ikiwemo vituo vya afya na shule hivyo kipaumbele changu cha kwanza tupate eneo hili kwa ajili ya shule na zahanati ” alisema Malisa .
Aidha Diwani Malisa pia ameliomba eneo la majengo ya SUDECO yatumike kwa ajili ya huduma za jamii kifuatia kuachwa majengo hayo zaidi ya miaka 20 bila kuendelezwa na kubaki magofu.
Alishauri eneo LA majengo ya SUDECO likipatikana watajenga vituo vya afya kutokana na Kata hiyo kuwa na wakazi wengi huduma za jamii wanakwenda Kata mama Kiwalani.
Akizungumzia maswala ya Ulinzi na Usalama alisema mikakati yake kupanua kituo kidogo ili kiwe cha kisasa waweze kupewa Askari .
Mikakati mingine Malisa alisema alisema anafanya mazungumzo na DAWASA Wilaya ya Temeke ili maeneo mengine yaweze kupata maji ya DAWASA kwa asilimia 100 .
Akizungumzia mradi wa kuboreshwa miundombinu DMDP Malisa alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamori na Serikali kwa usimamizi wa mradi huo ambapo kwa sasa anajivunia na wananchi wake.
Katika hatua zingine DIWANI Malisa ameomba Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam imtafutie Mkandarasi mwingine wa takataka kufuatia Mkandarasi aliopo Kata hiyo ametumia madaraka yake vibaya na kukosa sifa za kuwepo ndani ya Kata hiyo .
Mgeni rasmi Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto alimwomba diwani Malisa aandike barua rasmi kwa ajili ya mchakato wa kuomba wa kuomba eneo hilo ili litumike kwa ajili ya shule.
Meya Kumbilamoto alisema Serikali ya awamu ya tano inatekeleza mpango wa elimu bure hivyo lazima watoto wetu waweze kupata elimu .
“Taifa lolote ili liweze kuendelea lazima wananchi wake wasome tunaunga mkono juhudi za Rais wetu Samia Hassani Suluhu katika kusimamia sekta ya elimu na mwaka huu Halmashauri ya jiji imeweza kufaulisha watoto 27,000 kwenda sekondari.
Meya Kumbilamoto alisema mikakati ya Halmashauri hiyo kwa sasa wametenga shilingi bilioni 2 kwa ajili ujenzi wa madarasa eneo likipatikana.
Mwisho