Na: Mwandishi Wetu, TANGA.
Wito umetolewa kwa Wafanyabiashara na wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kwenye Banda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), lililopo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tanga ili kuweza kupata elimu ya namna ambavyo BRELA inavyofanya shughuli zake na kuweza kufanya maombi ya ujasili wa majina ya Biashara zao na kuweza kupatiwa Leseni zao za Biashara Papo kwa papo.
Wito huo umetolewa Mkoani Tanga na Afisa Leseni wa BRELA, Robert Mashika wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ushiriki wao kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Tanga yaliyofunguliwa rasmi Mei 28 Mei 28, 2021 na kufunguliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe kweye uwanja wa Mwahako Jijini humo.
Amesema endapo watashindwa kuelewa wawasiliane na BRELA kwa kupiga simu katika kituo chao cha miito ili kupata maelekezo ya kina na kwamba maombi ya leseni za biashara kundi A au maombi ya leseni za viwanda waingie kwenye tovuti ambapo wataweza kupata miongozo kwa urahisi
Kwa mujibu wa Mashika, BRELA wameshiriki kwenye maonesho hayo ili kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiriamali na watu ambao wameishaanza kufanya biashara, kuhuisha biashara zao.
Amesema tangu Mei 28 hadi Juni 6, 2021 watakuwa kwenye maonesho hayo kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali. Alitaja huduma ambazo zinapatikana kwenye banda hilo kuwa ni pamoja na kusajili makampuni, kusajili majina ya biashara, kusajili huduma na alama za biashara na utoaji wa hataza au vumbuzi na utoaji wa leseni za biashara kundi A.
Ametaja huduma nyiingine kuwa ni za utoaji wa leseni za viwanda, Uhuishaji wa taarifa za makampuni, ambayo yalisajiliwa kwenye mfumo wa zamani na kuyahuisha na kuyapeleka kwenye mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao (Online Registration Syestem).
Mashika ameongeza kwamba kupitia maonesha hayo, wanashauri washiriki na wananchi wote kwa ujumla wa jiji la Tanga na maeneo mengine kujitokeze kwa wingi kwenye maonesho hayo ili kusajiliwa biashara zao na kupata elimu ya kibiashara ambayo inatolewa na BRELA.
“Sisi BRELA ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na moja kati ya majukumu yetu ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ili wajue namna ya kufuata sheria za kibiashara,” amesema Mashika.
Amesema kwa sasa wafanyabiashara na wajasilianali hawana sababu ya kuhangaika kwa sababu huduma zao zote zinapatikana kwa njia ya mitandao kupitia tovuti za BRELA.
“Tunawashauri watu wa biashara na wajasiriamali kutembelea tovuti zetu ambazo ni rafiki wanaweza kufanya maombi yao au kupiga simu namba maalum ya kituo cha miito ili kupata maelekezo kama kuna changamoto zaidi,” amesema Mashika.
Akijibu swali lililohoji juu ya changamo gani ambazo wamebaini wananchi nakutana nazo kupitia maonesho hayo ya kimataifa ya Tanga, Mashika amesema kuwa watu wengi wamekuwa na changamoto ya utumiaji wa mifumo wa njia ya mtandao.
“Lakini pia kulikuwa na changamoto ya watu wa kati wanaojiita wakala wa BRELA, wakati ni vishoka, ambapo kuna wafanyabiashara ambao walidanganywa na hivyo kusajiliwa kwa vyeti feki.
Kwa hiyo tumewafuatilia wafanyabiashara hao na kuwapa vyeti halisi wakati tukiendelea na ufuatiaji wa watu hao walioghushi vyeti na saini vya maofisa wetu ili kuchukulia hatua za kisheria.”Amesema Mashika.