Home BUSINESS BRELA YARAHISISHA HUDUMA ZAKE, YASAJILI NA KUTOA VYETI PAPO KWA PAPO JIJINI...

BRELA YARAHISISHA HUDUMA ZAKE, YASAJILI NA KUTOA VYETI PAPO KWA PAPO JIJINI TANGA.

 

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (mwenye tai nyeusi) akipokea maelezo kuhusu usajili unaotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), kutoka kwa Afisa Msajili Msaidizi Bi. Maryglory, alipotembelea banda la Taasisi hiyo, kabla ya ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Biashara Tanga, yaliyoanza Mei 28, 2021, katika viwanja vya Mwahako jijini  Tanga. Maonesho hayo yaliyofunguliwa Mei 31, 2021 na Mhe. Kigahe,  yatahitimishwa Juni 6, 2021.

Bw.Ismail Salim (kushoto) akipokea cheti cha Usajili wa jina la Biashara kutoka kwa Afisa Usajili Msaidizi wa Wakala wa Usajili wa biashara na Leseni (BRELA), Bi. Maryglory Mmary (kulia) , baada ya kukamilisha taratibu za usajili kwa njia ya mtandao katika banda la BRELA kwenye Maonesho ya Biashara yanayofanyika katika uwanja wa Mwahako jijini Tanga. Maonesho haya yaliyoanza Mei 28, 2021 na kufunguliwa na Naibu Waziri wa  Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) yatahitimishwa rasmi Juni6, 2021

Afisa  Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)Bw. Robert Mashika (kulia), akimkabidhi cheti cha  usajili wa Jina la Biashra Bi. Afsa Jumanne Kwalo (kushoto),  katika banda la BRELA, mara baada ya kukamilisha taratibu za usajili  kwa njia ya mtandao,  kwenye maonesho ya Biashara Tanga, yanayofanyika katika uwanja wa Mwahako. Maonesho haya yaliyoandaliwa na Chemba ya Wafanyabishara , Viwanda na Kilimo  (TCCIA), yalifunguliwa rasmi Mei 31, 2021,  na yatahitimishwa Juni 6, 2021.


Wadau wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakiendelea kupata huduma mbalimbali katika banda la BRELA kwenye maonesho ya Biashara  yanayoendelea katika uwanja wa  Mwahako jijini Tanga. Maonesho haya yaliyoanza Mei 28, 2021 na kufunguliwa na  Naibu Waziri wa  Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb), yatahitimishwa rasmi  Juni 6, 2021.

 Na: Mwandishi Wetu, TANGA.

Wito umetolewa kwa Wafanyabiashara na wajasiriamali kujitokeza kwa wingi kwenye Banda la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), lililopo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tanga ili kuweza kupata elimu ya namna ambavyo BRELA inavyofanya shughuli zake na kuweza kufanya maombi ya ujasili wa  majina ya Biashara zao na kuweza kupatiwa Leseni zao za Biashara Papo kwa papo.

Wito huo umetolewa Mkoani Tanga na Afisa Leseni wa BRELA, Robert Mashika wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ushiriki wao kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Tanga yaliyofunguliwa rasmi Mei 28 Mei 28, 2021 na kufunguliwa na  Naibu Waziri wa  Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe  kweye uwanja wa Mwahako Jijini humo.

Amesema endapo watashindwa kuelewa wawasiliane  na BRELA kwa kupiga simu katika kituo chao cha miito ili kupata maelekezo ya kina na kwamba maombi ya leseni za biashara kundi A au maombi ya leseni za viwanda waingie kwenye tovuti ambapo wataweza kupata miongozo kwa urahisi

Kwa mujibu wa Mashika, BRELA wameshiriki kwenye maonesho hayo ili kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiriamali na watu ambao wameishaanza kufanya biashara, kuhuisha biashara zao.

Amesema tangu Mei 28 hadi Juni 6, 2021 watakuwa kwenye maonesho hayo kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali. Alitaja huduma ambazo zinapatikana kwenye banda hilo kuwa ni pamoja na kusajili makampuni, kusajili majina ya biashara, kusajili huduma na alama za biashara na utoaji wa hataza  au vumbuzi na utoaji wa leseni za biashara kundi A.

Ametaja huduma nyiingine kuwa ni za utoaji wa leseni za viwanda, Uhuishaji wa taarifa za makampuni, ambayo yalisajiliwa kwenye mfumo wa zamani na kuyahuisha na kuyapeleka kwenye mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao (Online Registration Syestem).

Mashika ameongeza kwamba kupitia maonesha hayo, wanashauri washiriki na wananchi wote kwa ujumla wa jiji la Tanga na maeneo mengine kujitokeze kwa wingi kwenye maonesho hayo ili  kusajiliwa biashara zao na kupata elimu ya kibiashara ambayo inatolewa na BRELA.

“Sisi BRELA ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na moja kati ya majukumu yetu ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali ili wajue namna ya kufuata sheria za kibiashara,” amesema Mashika.

Amesema kwa sasa wafanyabiashara na wajasilianali hawana sababu ya kuhangaika kwa sababu huduma zao zote zinapatikana kwa njia ya mitandao  kupitia  tovuti za BRELA.

“Tunawashauri watu wa biashara na wajasiriamali kutembelea tovuti zetu ambazo ni rafiki wanaweza kufanya maombi yao au kupiga simu namba maalum ya kituo cha miito ili kupata maelekezo kama kuna changamoto zaidi,” amesema Mashika.

Akijibu swali lililohoji juu ya changamo gani ambazo wamebaini wananchi nakutana nazo kupitia maonesho hayo ya kimataifa ya Tanga, Mashika amesema kuwa watu wengi wamekuwa na changamoto ya utumiaji wa mifumo wa njia ya mtandao.

“Lakini pia kulikuwa na changamoto ya watu wa kati wanaojiita wakala wa BRELA, wakati ni vishoka, ambapo kuna wafanyabiashara ambao walidanganywa na hivyo kusajiliwa kwa vyeti feki.

Kwa hiyo tumewafuatilia wafanyabiashara hao na kuwapa vyeti halisi wakati tukiendelea na ufuatiaji wa watu hao walioghushi vyeti na saini vya maofisa wetu ili kuchukulia hatua za kisheria.”Amesema Mashika.

Previous articleTBS YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA VIUNGO VYA VYAKULA JIJINI DAR ES SALAAM.
Next articleHATUTARUHUSU MTENDAJI ABAKI NA FEDHA AKISUBIRI MUDA WA NYONGEZA – WAZIRI MKUU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here