Home SPORTS AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 0:0 NA NAMUNGO FC RUANGWA.

AZAM FC YALAZIMISHWA SARE YA 0:0 NA NAMUNGO FC RUANGWA.

RUANGWA, LINDI.

TIMU ya Azam FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.


Sare hiyo inayoiongezea kila timu pointi moja, inaifanya Azam FC ifikishe pointi 64 baada ya kucheza mechi 32 sasa, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi tatu na Yanga ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati Namungo FC inafikisha pointi 43 za mechi 32 pia na inabaki nafasi ya tano,  ikizidiwa pointi sita na Biashara United.


Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, KMC imelazimishwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, timu ya Manungu mkoani Morogoro ikitangulia kwa bao la Kelvin Sabato dakika ya 55, kabla ya wenyeji ‘Watoto wa Kinondoni’ kusawazisha kupitia kwa Cliff Buyoya dakika ya 82.

Story, Na: Bin Zubeiry Blog.

Previous articleUONGOZI WA YANGA SC WATAJA AJENDA 12 ZA MKUTANO WAKE WA JUNI 27 MWAKA HUU.
Next articleRAIS DKT. MWINYI AZUNGUMZA NA MKURUGENZI MKUU WA BOHARI YA DAWA (MSD ) IKULU ZANZIBAR.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here