Home LOCAL WATUMISHI WA TAASISI ZA KANISA ANGLIKANA TANZANIA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA JUHUDI...

WATUMISHI WA TAASISI ZA KANISA ANGLIKANA TANZANIA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA JUHUDI NA MAARIFA

 Na: Maiko Luoga, TANGA.
Watumishi wa Taasisi za Kanisa Anglikana Tanzania wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma, ubunifu na maarifa ili kushiriki kutangaza injili ya Kristo kwa Jamii kupitia kazi zao ndani ya Kanisa.

Wito huo umetolewa mei 30, 2021 na Mhashamu Baba Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania na Dayosisi ya Tanga Dkt, Maimbo Mndolwa kwenye Ibada ya kuwaingiza kazini Watumishi wanaoenda kufanya kazi kwenye Taasisi za Kanisa Anglikana Dayosisi ya Tanga.

Katika Ibada hiyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu Mt, Michael Anglikana Korogwe Dayosisi ya Tanga jumla ya Watumishi tisa wa Sekta za Afya, Ustawi wa Jamii na Walimu wameingizwa kazini tayari kwa kutekeleza majukumu ya kuihudumia Jamii katika Dayosisi hiyo.

Akizungumza kwenye Ibada hiyo na kuwakabidhi Watumishi wapya kwa Wakuu wa Idara ikiwemo Afya na Elimu Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Maimbo Mndolwa amesema baadhi yao wataenda kufanya kazi katika Hospital za St, Augustine Muheza, St, Frances Kwamkono na Shule ya Sekondari Hegongo. 

“Tumefanya Ibada hii na kuwaingiza kazini kwa matazamio wale wakataokidhi vigezo tutawapa nafasi ya ajira hivyo mnatakiwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa pamoja na kufuata misingi na Sheria za Kanisa Anglikana” Dkt, Maimbo Mndolwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here