Home Uncategorized DKT. GWAJIMA AFANYA UFUATILIAJI WA MUONGOZO NAMBA 7 WA USHAURI WA WASAFIRI...

DKT. GWAJIMA AFANYA UFUATILIAJI WA MUONGOZO NAMBA 7 WA USHAURI WA WASAFIRI KIA.

Waziri Dkt.Gwajima akimpima joto msafiri aliyewasili nchini ikiwa ni hatua za awali za uchunguzi wa Afya za wasafiri.

Eneo maalum la kupima kipimo Cha haraka Cha Covid-19 (Rapid Test) kilichopo ndani ya uwanja wa ndege wa KIA ambapo wasafiri wanaowasili nchini hupimwa kabla ya kuanza taratibu zingine ndani ya uwanja


Mmoja wa wataam wa Afya waliopo Kwenye vyumba maalumu vya kupima kipimo Cha haraka Cha Corona akipima kipimo Cha haraka Cha Corona kutoka kwa msafiri aliyewasili nchini.

Waziri wa Afya Dkt.Dorothy Gwajima akiangalia utaratibu wa uchunguzi wa awali wa Hali ya afya za wasafiri (Primary health screening) Katika uwanja huo.

Waziri wa Afya akiwa na maofisa afya wakiangalia mfumo wa kieletroniki wa afya Msafiri ambapo msafiri hujaza ndani ya masaa 24 kabla hajaanza safari.

Maafisa afya wa uwanja wa ndege wa KIA wakiwa wamejitayarisha kutoa huduma kwa wasafiri wanaowasili nchini Kwenye uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro,ambapo leo Waziri wa Afya ametembelea kiwanja hicho.


Waziri wa Afya Dkt Gwajima akiingiza taarifa za msafiri Kwenye mfumo wa kieletroniki wa Afya Msafiri ili kujiridhisha jinsi unavyofanya kazi.

Na:Catherine Sungura,WAMJW-Kilimanjaro.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, leo ametembelea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ikiwa ni kufuatilia utekelezaji wa muongozo namba 7 wa ushauri wa wasafiri  wanaoingia nchini uliotolewa tarehe 4 Mei, 2021.

Katika muongozo huo moja ya maelekezo ni kufanya uchunguzi wa COVID-19 kwa  kuwapima kipimo  cha haraka (Rapid Test) wasafiri wote wanaoingia nchini, kwani kumekuwa na malalamiko kadhaa kutoka kwa wananchi kuhusu zoezi hilo. Mojawapo ya malalamiko hayo ni abiria kuchelewa kumaliza hatua za huduma ya vipimo vya afya.

Mhe. Waziri amebaini kuwa watumishi wapo na wanafanya kazi zao vizuri wakiwemo maafisa afya, maabara na watumishi wa uwanja wa ndege. Waziri amewapongeza watumishi hao kwa kazi nzuri wanaoifanya. Aidha, amewashukuru viongozi wa mkoa wa Kilimanjarao na Halmashauri ya Hai, Moshi kwa kutoa watumishi wa ziada ili kuongeza nguvu.

Amesema kuwa abiria kuchelewa kumaliza hatua za vipimo vya afya pia inachangiwa na baadhi yao kutojaza taarifa zao za hali yao ya afya kupitia mfumo wa kieletroniki wa afyamsafiri ambao unamtaka abiria kujaza taarifa zake ndani ya masaa 24 kabla ya kuingia nchini na hivyo kuwafanya wachelewe kuanza hatua ya uchunguzi wa awali (primary screening) na mwisho kufanya hatua zote za kulipia na kupima kuchelewa pia.

Aidha, ametoa wito kwa mashirika ya ndege na mamlaka ya viwanja vya ndege, usafiri wa ndege na wakala wa ndege, mabasi kushirikiana kutoa elimu ili taarifa hizo zijazwe mapema kabla ya kufika katika maeneo yetu ya viwanja vya ndege, bandari na mipaka yote.

Kwa upande wa vipimo vya awali ameelekeza ufanyike utaratibu wa kuongeza idadi ya wapimaji kutoka watano hadi kufikia 8 na wakati huo uratibu ufanyike kuomba wahasibu kutoka wizara ya fedha kwa ajili ya kuratibu malipo kwa ushirikiano na banki husika na wataalamu wa afya wahusike na kuongeza nguvu ya kutoa huduma za afya.

Pia kwa kuzingatia kuelekea msimu wa wageni wengi wizara itashirikiana na wadau wake kuimarisha huduma za vipimo vya haraka huku ikiendelea kupokea maoni mbalimbali na kuyafanyia kazi. Vilevile, amesema wizara itaendelea kuboresha mfumo wa afyamsafiri ili uweze kurahisisha taratibu za kuwahudumia wasafiri kabla hawajaanza safari na kupunguza changamoto mbalimbali wanazolalamikia wakati wanapowasili nchini.

Previous articleTANZANIA NA KENYA ZAKUBALIANA KUONDOA VIKWAZO 30 VYA BIASHARA VISIVYO VYA KIUSHURU, VIKWAZO VINGINE 34 VIPO KWENYE MKAKATI WA UTEKELEZAJI.
Next articleWATUMISHI WA TAASISI ZA KANISA ANGLIKANA TANZANIA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA JUHUDI NA MAARIFA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here