wakili wa kujitegemea peter madeleka ameitaka serikali kuendelea na uchunguzi wa ku watafuta wahusika wa viza za kughushi baada yawakili huyo kuwa muhanga kwa kukaa mahabusu zaidi ya mwaka moja kwa shitaka la hujumu uchumi hatimaye kuachiwa uhuru baada ya kufanya makubaliano na mwendesha mashitaka
akiongea na vyombo vya habari wakati akielezea kusihuana na suala hilo wakili madeleka amesema tangu alivyo kamatwa kwa kosa la kughushi tahere 14 oct 2019 amejifunza kwakuona baadhi ya taratibu za sheria za uendeshaji wa kesi za ujuhumu uchumi zinakiukwa na kupelekea msongamano mkubwa kwenye mahabusu ikiwemo tatie
akielezea baadhi ya taratibu ambazo amedai zina kiukwa madeleka amesema taratibu hizo ni pamojana za mwanzo ambazo zinakiukwa ni kifungu 21(1) ambacho kina sema lazima gazeti la serikali litangaze amri ambayo inatoa ruhusa ya upelelezi huo kufanyika ikwemo uhalali wa waendesha mashitaka kutangzwa kwenye magazeti ya serikali kama kifungu na 25(1) kinavyo taka suala ambalo amesema linatoa mwanya kwa upelelezi kuto kamilika
Aidha madeleka ametaka serikali ifanyeuchunguzi upya wa tuhuma za kughushi viza na yuko tayari kutoa ushirikiano kuweza kuwa baanisha wa uhusika wa suala hilo hatahivyo ameshukuru kwa hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya sita katika kuingalia upya sheria hiyo