Home BUSINESS WACHIMBAJI WADOGO WANAMCHANGO MKUBWA WA KUKUZA UCHUMI WA TANZANIA.

WACHIMBAJI WADOGO WANAMCHANGO MKUBWA WA KUKUZA UCHUMI WA TANZANIA.

 

Na:Simon Mghendi, Kahama

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kuwa wachimbaji wadogo wa madini nchini wamekua na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa.

Biteko ameyasema hayo  Wakati akikabizi leseni za uchimbaji wa madini kwa wachimbaji wadogo katika mgodi wa Mwabomba uliopo halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Pia biteko alitumia fursa hiyo kuwaasa wachimbaji wadogo nchini kuacha majungu na kuoneana wivu wao kwa wao na badala yake washikamane ili waweze kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wao wachimbaji wadogo wameishukuru serekali kupitia wizara ya madini kwa kuwapa leseni, jambo ambalo litapelekea kufanya kazi kwa kujiamini na kuongeza mapato ya nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here