Home LOCAL THBUB YAMPONGEZA MHE. RAIS SAMIA KWA KUTOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 5000.

THBUB YAMPONGEZA MHE. RAIS SAMIA KWA KUTOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 5000.

 

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora (THBUB) Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akizzungumza na waandishi wa habari 

Na: Hughes Dugilo.

Tume ya Haki za Binaadamu na utawala Bora (THBUB) imempongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kufuatia msamaha alioutoa kwa wafungwa 5’001 waliokuwa wakikabiliwa na vifungo mbalimbali.


Katika taarifa yake iliyotolewa Mei 8,2021 na kusainiwa na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu imesema kuwa Tume inachukulia atua hiyo ya Rais kama jambo ambalo linaweka nguvu na mkazo  katika sehemu ya majukumu yake ya kuhakikisha haki za binadamu zinafatiliwa na watu wote ikiwemo wale walio magerezani. 


“Tume inaunga mkono kauli aliyotoa Mheshimiwa Rais ya kuwataka wafungwa walioachiwa huru kutumia vema mafunzo waliyoyapata wakiwa gerezani waungane na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa huku wakiheshimu na kuzingatia Sheria” amesema Jaji Mwaimu.


Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 ibara 25(1) (a), na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ibara ya 22(1) (a) kila mtu anao wajibu wa kushiriki katika kazi halali ya uzalishaji mali.


Wakati huo huo ibara ya 26(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ibara ya 23(1) ya katiba ya Zanzibar inatoa wajibu kwa kila raia kutii sheria za Nchi.


“Ni matumaini ya Tume wafungwa walioachiwa na wananchi wote kwa ujumla watazingatia wito huu wa Mheshimiwa Rais kwa manufaa ya Taifa letu” amesisitiza.


Aidha Tume imeishauri jamii na wanufaika wa msamaha wa Mheshimiwa Rais kuwa wafungwa walioachiwa huru wakayatumie mafunzo na maarifa waliyoyapata wakiwa gerezani katika kazi za uzalishaji mali na kujipatia kipato, pia wale waliopunguziwa adhabu zao  wawe na mwenendo mazuri ili atimaye nao waweze kuachiwa huru kwani Tume inaamini hiyo ndio njia pekee ya kumpa faraja Mheshimiwa Rais kwa uamuzi wake.


Pia Tume inawasihi watanzania wote kuweza kuwapokea ndugu zao kwa mtazamo chanya na kushiriana nao katika ujenzi wa Taifa.


Itakumbukwa kuwa April 26 2021 siku ya maandhimisho ya miaka 57 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alitangaza msamaha kwa wafungwa 5,001 waliokuwa wakikabiliwa na adhabu ya vifungo mbalimbali.

Previous articleYANGA YAWEKA MSIMO KUSOGEZWA MUDA WA MCHEZO WAO NA SIMBA.
Next articleRAIS SAMIA AZINDUA KITABU CHA HISTORIA YA MAISHA YA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MZEE ALI HASSAN MWINYI JIJINI DAR ES SALAAM.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here