Home LOCAL TABATA KIMANGA WAZINDUA USAFI.

TABATA KIMANGA WAZINDUA USAFI.

 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sokoine Kata ya KIMANGA Sharifa Oreme (Katikati)akiongoza Kampeni ya uzinduzi ya Usafi Leo Mei 30/2021 (PICHA NA HERI SHAABAN).

Viongozi wa Serikali ya Mtaa Sokoine KIMANGA wakizindua usafi kwa kusafisha Mitalo Kituo cha Daladala KIMANGA Leo Mei 30/2021 .(PICHA NA HERI SHAABAN)

Wananchi wa Mtaa wa Sokoine KIMANGA wakisafisha mitalo Leo Mei 30/2021 katika uzinduzi wa Usafi (PICHA NA HERI SHAABAN).

NA: HERI SHAABAN,DAR ES SALAAM.

SERIKALI ya Mtaa wa Sokoine wamezindua Kampeni endelevu ya Usafi katika mtaa huo kwa kufanya usafi maeneo mbalimbali.

Akizindua Kampeni hiyo ya Usafi Mwenyekiti wa Mtaa Sikoine Sharifa Oreme , alisema Kampeni hiyo ni endelevu amewataka wananchi watunze mazingira yao kwa Usafi.

“Tumezindua Kampeni endelevu ya Usafi mtaani kwetu pamoja na kituo cha Daladala KIMANGA nawaomba wananchi wangu wa Kimanga tuhamasishane na kutoa elimu ya Usafi.

Sharifa alisema wananchi watakaochafua mazingira na kufuata za usafi watachukuliwa hatua ikiwemo kutozwa faini ili wafuate sheria za usafi 

Aliwataka wananchi kujenga tabia ya kuwa wasafi kila wakati kwa kutunza mazingira yao yanayowazunguuka .

Sharifa alisema kila Jumamosi KIMANGA ni siku ya usafi pamoja na mwisho wa mwezi kwa wafanyabiashara na Wananchi .

Aidha alisema Jumatatu Mei 30/2021 Daladala zote za KIMANGA zinatakiwa kushusha abiria KIMANGA mwisho kituoni Daladala zitakazokiuka sheria zitachukuliwa hatua na Mamlaka husika.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here