Home LOCAL SERIKALI KUPANUA WIGO WA INTERNET NCHINI KUANZIA 3G KWENDA JUU-WAZIRI DKT NDUNGULILE

SERIKALI KUPANUA WIGO WA INTERNET NCHINI KUANZIA 3G KWENDA JUU-WAZIRI DKT NDUNGULILE

WAZIRI wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Mhe Dkt Faustine Ndungulile akijibu baadhi ya hoja za Wabunge Bungeni Jijini Dodoma

Mbungewa Viti Maalumukupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Mhe Neema Lugangira akisisitiza jambo  bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia

 NA: MWANDISHI WETU, DODOMA.

WAZIRI wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Mhe Dkt Faustine Ndungulile amesema Serikali itaongeza wigo wa Internet nchini na minara yote itakuwa
inajengwa  kuanzia  3G kwenda juu ili kuwawezesha watanzania walio wengi
waweze kupata huduma ya mtandao mpaka wananchi wa vijijini ili kuweza
kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ili kuweza kujiletea maendeleo
yao.

Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Mhe Neema Lugangira ambaye aliishauri Serikali ipanue wigo wa Mtandao wa Internet ili wananchi wa
mikoa ya pembezoni na vijijini nao waweze kunufaika na fursa
zinazotokana na huduma hiyo.

Dkt Ndungulile alisema mwanzoni walipokuwa wanaanza mikakati yao
ilikuwa ni kuhakikisha mawasiliano maana mitano yote ilikuwa ni 2G hivyo
wamekubaliana kwa sasa minara yote inayokwenda kujengwa inakuwa 3G
kwenda juu.

Alisema kwani Dunia hivi sasa inaongelea masuala ya Digital Economy na ukiangalia miaka 10 iliyopita makampuni makubwa duniani yalikuwa kwenye
manufacturing lakini sasa hivi ukiangalia yapo kwenye sekta ya Tehama
hivyo kama nchi lazima waangalie huko.

“Kujibu swali hili la Mhe Neema Lugangira tupo kwenye maandalizi ya kuandika Digitali Economy Blue Print ya Tanzania na kazi hiyo imeshaanza hatua za awali na tunatarajia andiko litaanza hivi karibuni, sambamba na kuangazia e-commerce ”Alisema Mhe Dkt. Ndugulile.

Waziri huyo hataki kukumbukwa kwamba alikuwa akiminya Sera ya Sekta hiyo
badala yake akumbukwe kwa kufanya mazingira wezeshi ya Tehama kukua
ndani ya nchi lakini niwaambie Wabunge kwamba tunakwenda kufanya
mabadiliko makubwa sana ya kimuundo ya taasisi zake na muundo wa
kisheria.

Alisema ikiwemo pamoja na vijana wanaojiajiri kupitia Tehama kwa vijana  akitolea mfano nvijana ambao ni ni MC anafanya shughuli za harusi anarusha picha
youtube ili watu waione umahiri wake wa kazi halafu anataka kutozwa kodi
hilo wanataka kulikataa.

Aidha alisema pia wasanii wanatoa kazi zao wanaziweka kwenye mitandao wao
wanakwenda kuwaminya wanataka kwenda kufanya maboresha makubwa ambayo yataweka mazingira wezesehi kuhakikisha platfomu zao hawawezi kuzuia bali wawe wanakwenda ili vijana hao waweze kujiajiri.

Katika hoja yake pia Mbunge Neema Lugangira aliishauri Wizara kuona mana gani itaweza kupunguza ghamara zinazolipwa na Watanzania hususani hawa vijana kwa sababu hivi sasa ni changamoto kubwa. 

Pia aliitaka Wizara ifanye mapitio ya sheria ili kuona namna gani ya
kuondoka baadhi ya makosa kutoka makosa ya Jinai kuwa makosa ya madai
maana yenyewe inaleta changamoto kubwa sana kuhakikisha watu wamenufaika
na sekta hiyo.

“Lakini pia waongeze eneo la ufikaji wa internet kama wengine walivyochangia hususani vijijini hata wakifikie 3G kwa sababu interneti inasaidia kufanya biashara kwa vijana na wanawake na ukiingia mtandao waInstragamu inasaidia sana lakini fursa hizo haziwasaidia wanaotoka
maeneo ya pembezoni”

Mhe Neema Lugangira alisema pia lakini bado gharama za kupata internet hapa nchini ni kubwa ukilingananisha na nchi jirani mfano Nairobi gharama ya
uzito kwa mwezi ni Dola za Kimarekani 5.5, Uganda kwa maana mji wa
Kampala ni Dola za Kimarekani 10 na Tanzania kwa maana Dar es Salaam ni
Dola za Kimarakeni 15.5 kwa hiyo unaweza kuona ulinganishi huu hivyo ni
muhimu kufanya uangalizi wa gharama hizo.

Aliongeza kwa hali ilivyo watanzania wengi hawafaidi na hawanufaiki na sekta hiyo na Wizara ikiweza kufanyia kazi ushauri anautoa wataipunguzia mzigo
Serikali wa ajira kwa vijana kwa sababu vijana watatumia Sekta hii
kujitengeneza ajira.

“Natoa shukurani kwa Rais Samia Suluhu Hassam kutokana na mwongozo na nia yake kuhakikisha miundombinu ya teknolojia ya mawasiliano inafika asilimia 80 ifikapo mwaka 2025 hayo ni maono makubwa ambayo yatapelekea
kuimarisha uchumi wetu zaidi eneo la teknoloji ya mawasiliano”
Alisema
Mbunge Neema Lugangira.

Alisema kwa sababu ni sekta muhimu ambayo ikiangaliwa kwa umakini nchi inaweza kupata kipato kikubwa pamoja na kutengeneza ajira  akitolea mfano Kenya sekta ya teknolojia ya mawasiliano inachangia asilimia 8 ya pato ghafi
la Taifa na tayari sekta hiyo kwa Kenya imeshatengeneza ajira 250,000 na
hiyo ni kwa mujibu wa Takwimu ya Serikali ya Kenya.

Mbunge Neema Lugangira alisema ukuaji wa sekta ya ICT Kenya umepitia ukuaji mkubwa kupita sekta zote kwa zaidi ya asilimia 23 na hiyo ni kwa mlongo
uliopita pekee lakini kwetu Tanzania bado kuna changamoto ambazo
wakiziangalia vizuri zitasaidia kuongeza ajira kupitia sekta hiyo ambazo
hivi sasa imefungwa.

“Mfano mdogo wachangiaji wengi asubuhi walizungumzia suala la Youtube hivi sasa kwa Tanzania mazingira yake sio rafiki nasema hivyo kwa sababu wapo wana mziki wachache au wadau ambao wanatumia YouTube akiwemo Diamond, Alikiba na Milladayo ambao wamenufaika lakini baada ya kuwepo kwa sheria ambazo zimepelekea changamoto watu wengi wamejiondoa kutumia mtandao huo ikiwemo vijana” Alisema.

Mhe Neema Lugangira alisisitiza kuwa hiyo inaleta changamoto kubwa kwa
sababu vijana wanatumia teknologia hiyo na sekta hiyo kujipatia ajira
ambazo ni changamoto hivyo Sera zetu lazima ziweke Mazingira ya
kuwawezesha wao kujiajiri.

Aliendelea kusema “Pamoja na changamoto hizo tofauti na nchi zingine hapa Tanzania vijana wetu wengi waliopo kwenye sekta hiyo hawana elimu rasmi ya masuala ya kidigitali hivyo tunavyowaongezea gharama za kulipa ni
kufifisha jitihada zao binafasi ambazo wamezichukua kama vijana
kujitengeneza ajira”
Alisema.

Mbunge Neema Lugangira alisema katika hili naomba niishukuru Kamati maana nao wamelisemea hilo na ushauri wangu wa tano naiomba Serikali iangalia namna ya kushirikiana na wabunifu ili kuongeza faida inayopatikana
kupitia sekta hiyo waone namna gani ya kuweza kushirikiana nao na kuomba
Wizara isijifungie na katika hilo naomba nimpongze Mh Spika, Mhe Job
Ndugai kwa jithada zake kufungua milango ambapo alieleza awali Mhe Spika
alikutana na vijana ambao ni wabunifu wakatengeneza app iliyokuwa
inawezesha vijana na wananchi kuwa karibu na wabunge wao hivyo wizara
ikishirikiana na hao wabunifu inaweza kuleta tija.

Hata hivyo alisema kwa kumalizia wanaweza kujifunza kwa wenzetu wa Kenya
ambao wana Sera ya Digital Economy Blueprint ambapo hivi sasa Tanzania
hatuna Sera yeyote na hivyo aliishauri Wizara iandae  Sera Madhubuti ya Digital Economy Blueprint mengi yatashindikana maana hii sekta inahitaji iwe na miongozo thabiti lakini iwe na njia ambazo zitahakikisha inawalinda  watumiaji na walaji wa sekta hiyo alimuomba Mhe Waziri anapokuja kuhitimisha Hoja yake ya Bajeti ya Wizara yake aeleze ana mpango gani wa kuja na Sera ya Digital Economy Blueprint.

 

 

Previous articleRAIS SAMIA WA TANZANIA NA RAIS MUSEVEN UGANDA WATIA SAINI UJENZI BOMBA LA MAFUTA DAR.
Next articleNIC WADHAMIN DAR CITY MARATHON.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here