Home ENTERTAINMENTS NANDY AZINDUA MSIMU WA PILI TAMASHA LA ‘NANDY FESTIVAL’ 2021

NANDY AZINDUA MSIMU WA PILI TAMASHA LA ‘NANDY FESTIVAL’ 2021


DAR ES SALAAM.
DIVA wa muziki wa Bongo fleva nchini, Faustina Mfinanga, ‘Nandy’ amezindua msimu wa pili  wa tamasha la Nandy Festival kwa mwaka 2021 na safari hii atakiwasha hadi Kenya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Nandy amesema kuwa tamasha hilo litafanyika mikoa saba ya Tanzania na pia nchi jirani ya Kenya litafanyika Nairobi na Mombasa.

“Nandy Festival mwaka huu inakuja kivingine na itafungua ukurasa mpya kwa vijana wote wenye uthubutu na hii sio yangu peke ni fursa ya sisi wote kama vijana nikimaanisha wasanii na wafanyabiashara hasa wadogo wadogo tutakao kutana nao mikoani kwenye tamasha, amesema Nandy”.

Ameongeza kuwa tamasha hilo kwa hapa Tanzania litaanzia Kigoma June 5, 2021 na kutakuwa na wasanii mbalimbali akiwamo Billnass.
Previous articleRAIS SAMIA KUTARAJIWA KUWA MGENI RASMI BARAZA LA IDDI MWAKA HUU.
Next articleMNEC HAPPINESS MGONGO AWATAKA VIJANA KUMSAIDIA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here