Home LOCAL MNEC HAPPINESS MGONGO AWATAKA VIJANA KUMSAIDIA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN

MNEC HAPPINESS MGONGO AWATAKA VIJANA KUMSAIDIA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN

Na:Halfani Akida.

Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa, Bi. Happiness Mgongo amewataka vijana wa Chama Cha Mapinduzi na Tanzania kwa ujumla kumsaidia kumuunga mkono na kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi na kulinda rasilimali za Taifa.

“Tumuunge mkono Mhe. Rais wetu kulinda rasilimali za Taifa ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa maslahi ya Taifa la Tanzania, ametuamini sana sisi vijana na sisi tumuaminishe kuwa tunaweza”

Bi. Mgongo ameyasema hayo katika uchaguzi wa nafasi ya kumpata mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM)  mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ihemi.

Pia Bi. Mgongo amesema Taifa limepata kiongozi shupavu anayejali maishanya Watanzania na kutaka kuhakisha wananchi wanakuza vipato vyao, hivyo ni muhimu kuunga mkono juhudi hizo ili kufikia malengo kwa pamoja.

“Rais wetu Mama Samia Hassan ni mwanamke Jembe na shupavu, ameanza kutuonesha hilo kwa matendo na kutujengea imani kwamba tupo salama na tutavuka salama akituongoza yeye. Nia yake ni kuboresha maisha ya Watanzania

Katika hatua nyingine Bi. Mgongo amesema vijana wanayosababu ya kuchagua viongozi wawatakao bila kuyumbishwa kwa misingi ya Rushwa au namna yoyote bali uwezo binafsi wa viongozi ili kuwaletea maendeleo vijana wa mkoa wa Iringa.

“tusiwachague viongozi kutokana na pesa zao bali uwezo wao binafsi katika kutuunganisha sisi vijana na kusaidia kukuza vipaji na kipatomcha vijana ambao anawaongoza”

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwa kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 300 kutoka wilaya zote za mkoa wa Iringa, Arnold Mvamba ameibuka kidedea kwa kupata jumla ya kura 181, Fatma Ally Rembo kura 123 na Isack Mgovano kura 25.
Previous articleNANDY AZINDUA MSIMU WA PILI TAMASHA LA ‘NANDY FESTIVAL’ 2021
Next articleNTD IMEJIPANGA KUTOKOMEZA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE IFIKAPO 2030

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here