Home LOCAL MKURUGENZI MTENDAJI LHRC AWAFUNDA VIJANA DAR NA PWANI

MKURUGENZI MTENDAJI LHRC AWAFUNDA VIJANA DAR NA PWANI

 

Mtendaji Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Anna Henga (katikati) akizungumza na vijana alipokuwa akifungua Kongamano la Vijana toka Vyuo Vikuu, Vyuo vya Kati na Sekondari jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na Club inayohamasisha Elimu na Maadili kwa Vijana (EEMC) Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Mtendaji Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Anna Henga (wa kwanza kushoto) akimkabidhi zawadi ya kitabu cha ‘UBUNIFU’ mmoja wa vijana aliyemvutia kutokana na kipaji chake cha sanaa kwenye kongamano la vijana toka vyuo vikuu, vyuo vya kati na sekondari jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na Club inayohamasisha Elimu na Maadili kwa Vijana (EEMC) Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Mmoja wa vijana akiuliza swali kwenye Kongamano la Vijana toka Vyuo Vikuu, Vyuo vya Kati na Sekondari jijini Dar es Salaam.

 Sehemu ya washiriki wa kongamano hilo pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa LHRC.


MKURUGENZI Mtendaji Kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Anna Henga amewataka vijana kuwa na malengo
katika maisha yao na kuhakikisha wanafanya jitihada za kuyasimamia ili yaweze
kutimia. Mkurugenzi huyo ameyasema hayo jana alipokuwa akifungua kongamano la
vijana toka vyuo vikuu, vyuo vya kati na sekondari jijini Dar es Salaam
lililoandaliwa na Club inayohamasisha elimu na maadili kwa vijana (EEMC).

Alisema kijana mwenye malengo hana
budi kuweka jitihada katika kuyakamilisha na kutokubali kukata tamaa hata kama
anakumbana na vikwazo fulani kwenye maisha yake. “Kijana mwenye malengo
hana budi kung’ang’ania malengo yake katika kuyakamilisha, usikate tamaa wala
kukubali kushindwa kirahisi,” alisema Bi. Henga akiwasilisha mada yake kwa
vijana hao.

Aliwataka vijana kutumia changamoto
wanazokutana nazo kama fursa za mafanikio kuelekea katika malengo yao.
Ameongeza kuwa hata yeye katika mafanikio yake amekuwa akitumia vikwazo kama
fursa kukamilisha malengo jambo ambalo linawezekana kwa vijana endapo watafanya
maandalizi na jitihada kukamilisha malengo yao.

“..Jambo la msingi ni kufanya
maandalizi kuelekea kukamilisha malengo yako, tujiandae na tufanye kazi kwa
bidii na sisi ambao tunasoma tusome kwa bidii sana hakuja jambo zuri linalokuja
kirahisi bila kufanya jitihada wewe binafsi..pia tusikubali kupoteza muda ‘keep
time’…,” alisisitiza Mkurugenzi huyo Mtendaji wa LHRC.

Alisema kijana mwenye malengo
anatakiwa kujenga mahusiano mazuri na watu mbalimbali (networking)  jambo ambalo linaweza kumsaidia mbeleni
kuelekea kukamilisha malengo yake, hivyo kuwataka vijana kuto puuza mahusiano
mazuri na watu.

Pamoja na hayo aliwataka vijana kuwa
waadilifu na wacha Mungu katika kila jambo wanalolifanya kwani ni moja ya
daraja la mafanikio kuelekea kutimiza ndoto zao. Unapokuwa mwadilifu na
kumshirikisha Mungu mbele kwa kila jambo lako huwezi kushindwa kamwe, siku zote
utafanikiwa katika jambo lako,” alisisitiza kiongozi huyo.

Kwa upande wao mmoja wa waratibu wa
mkutano huo, David Sospita alisema kongamano hilo kubwa la vijana toka vyuo
vikuu, vyuo vya kati na sekondari lililoandaliwa na taasisi ya EEMC toka Dar es
Salaam na Pwani na kupewa kauli mbiu ya ‘kijana na malengo’ limelenga
kukutanisha vijana kuwaelimisha na kuchagiza malengo yao.

Alisema limeandaliwa ili kuchochea
hamasa ya elimu, elimu dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi, elimu ya
kujitegemea kwa vijana na pamoja na uongozi na maadili kwa vijana. Aliongeza
katika kongamano hilo  linalofanyika Chuo
Kikuu cha Muhimbili Dar es Salaam vijana watanolewa namna ya kujiajiri na
kutimiza ndoto za malengo yao.

Previous articleZAIDI YA WANANCHI ELFU 27 WAPATIWA ELIMU KUHUSU UBORA WA BIDHAA KWENYE WILAYA YA KILOSA,MKINGA NA BAGAMOYO.
Next articleMAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE SHEREHE YA KUMUWEKA WAKFU ASKOFU WA ANGLIKANA MWANZA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here