Home ENTERTAINMENTS MISS PWANI YAKARIBISHA WADHAMINI.

MISS PWANI YAKARIBISHA WADHAMINI.

Na:Mwandishi wetu.

MUANDAAJI  wa shindano la urembo mkoani Pwani, Maryam Ahmed ambaye ni mmilikiwa wa kampuni ya Twiga Entertainment, anawakaribisha wadau mbalimbali kujitokeza kudhamini shindano hilo mwaka huu.

Maryam Ahmed ‘Twiga’ ni moja ya wadua wakubwa wa shindano la urembo hapa nchini amewahi kutwaa mataji mbalimbali ya urembo ikiwemo miss Arusha mwaka 2007, na miss Kisura 2008.

Akizungumza na wandishi wa habari Twiga, amesema anakaribisha makampuni ambayo yanaweza kuungana nae kufanya shindano hilo ambalo limeibua viongozi na vipaji mbalimbali  vya wasichana hapa nchin.

“Nichukue nafasi hii kuwaomba wadau na serekali kuungana nami kufanikisha mchakato wa kumpata mrembo atakaye wakilisha mkoa wetu katika shindano la taifa na ambaye naamini atakuwa mrembo wa Taifa ,” anasema Twiga.

Aliongeza kuwa tayari mchakato wa kuwapata washiriki umesha anza na mwishoni mwa mwezi Mei wanatarajia kufanya uzinduzi mkubwa kama ilivyo kawaida ya mkoa huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here