Home LOCAL MADIWANI WAASWA KUWA DARAJA KATIKA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI 2020-2025.

MADIWANI WAASWA KUWA DARAJA KATIKA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI 2020-2025.



DODOMA.
Madiwani wa watokanao na Chama Cha Mapinduzi nchini wameaswa kuwa daraja la utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-25 kutokana na ukaribu wao kwa wananchi.

“Ndugu zangu Waheshimiwa Madiwani, nawaomba tutambue jukumu la kusimamia utekelezaji wa ilani ni la kwetu kwani sisi ndio tunapaswa kumsaidi Rais wetu Mh Samia Suluhu Hassan. Sisi tuwe daraja au kiunganishi katika utekelezaji”

Hayo yamesemwa leo tarehe 26 Mei, 2021,na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Ndg. Happiness Mgongo katika mkutano wa madiwani wa Chama Cha Mapinduzi nchini uliofanyika katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Taifa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama hicho Jijini Dodoma.

Bi. Mgongo amesema madiwani wanayo nafasi kubwa katika kuhakikisha Taifa linapata maendeleo kwa kuwa na ushiriki mzuri katika kupanga mapato na matumizi pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo katika vikao vyao vya Halmashauri nchini. 

“Mna nafasi kubwa ndugu zangu katika kusimamia maendeleo nchini, kwa kuwa nyie ndiyo wapitishaji wa bajeti katika halmashauri zenu na ndiyo washauri wakuu wa mawazo ya wananchi katika ngazi ya Halmashauri”

Katika hatua nyingine, Ndg. Mgongo amewataka madiwani nchini kuwa wazalendo na Taifa lao ili kujenga nchi hususani katika kipindi hiki ambacho Nchi imeingia katika majaribu kwa kupoteza kiongozi wa Nchi akiwa madarakani.

“Nchi yetu itajengwa na Wazalendo, pale penye kushauri ifanyike kwa busara zaidi na hoja zenye tija lengo ni kushikana mkono na Rais wetu  Mh. Samia Suluhu Hassan ili kusogeza huduma kwa Wananchi”

Aidha, Ndg. Mgongo amempongeza katibu mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Tanzania (UWT), Mama Queen Mlozi kwa namna ambavyo amekuwa mlezi mzuri kwa vijana katika Chama pamoja na kuonesha taswira anayotakiwa kuivaa kiongozi katika jamii.

“Kwa dhati ya moyo wangu kabisa.  Nampongeza Mama yangu Queen Mlozi Katibu UWT Taifa. Amekuwa mlezi mwema sana.Wanawake wa TZ tuna kila sababu ya kujivunia Madini tunayopokea kwake. Weledi Maadili na uelewa wake kwa CCM na Jumuiya ya Wanawake ni mtaji mkubwa kwa Taifa letu na vizazi vyetu.”

Mgongo ameahidi kushirikiana na madiwani wa CCM Nchini kufanya kazi na kuhakikisha Wananchi wote wanapata wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao ndiyo wenye Uhitaji zaidi wa maendeleo wanatimiziwa haja yao.

“Tumepokea mawazo na maoni yenu. Ndani ya CCM kuna vikao miongozo maelekezo taratibu na kanuni katika kufanya maamuzi. Hivo basi ondoeni shaka twendeni tukachape kazi”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here