Home BUSINESS WAKAGUZI WA NDANI BARA LA AFRIKA WAKUTANA JIJINI ARUSHA.

WAKAGUZI WA NDANI BARA LA AFRIKA WAKUTANA JIJINI ARUSHA.

Mwenyekiti wa Taasisi ya wakaguzi bara la Afrika(AFIIA) Emmanuel Johanes akioongea na waandishi wa habari katika mkutano wao wa saba.

Jafary Kachenje Mkaguzi mkuu wa ndani wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki akiongea na waandishi jiji Arusha.

NA:NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Wakaguzi wa Ndani Bara la Arika wamekutana jijini Arusha kujadili matumizi ya teknolojia katika utendaji kazi itakayowawezesha kuboresha ukaguzi wao kwa kupitia teknolojia.

Akifungua Mkutano wa 7 wa Wakaguzi wa Ndani wa Afrika (AFIIA) Mwenyekiti wa Taasisi ya wakaguzi hao Emmanuel Johanes alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuleta manufaa katika uchumi wa nchi za Afrika.

Johanes alisema kuwa  pia wataweza kujadili changamoto mbalimbali za wakaguzi na kujua jinsi ya kusaidia kuchangia maendeleo ya nchi za Afrika

pamoja na suala zima la kuboresha uwezo wa wakaguzi na kujifunza kutoka nchi zingine.

“Hapa tutabadilisha uzoefu kila mmja atajua nchi nyingine wanafanya nini na ni namna gani na sisi tunaweza kuboresha mikakati mbalimbali ya kupiga hatua katika maendeleo ya kiuchumi.”Alisema Johanes

Alifafanua kuwa zipo changamoto mbalimbali za kiutandaji,uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi pamoja na changamoto za bajeti za kuwezesha kazi kufanyika ambapo katika sekta ya umma bado wakaguzi wana changamoto nyingi kutokana na kutokuwa na bajeti na vifaa pamoja na mafunzo ya kutosha.

Kwa upande wake Jafary Kachenje Mkaguzi mkuu wa ndani wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki alisema kuwa ili kuweza kuepuka changamoto ambazo hutokea mara kwa mara,mafunzo ambayo wakaguzi wa ndani hupatiwa yanapaswa kutolewa kwa wakurugenzi na kwa kufanya hivyo yatawasaidia kufahamu umuhimu wa wakaguzi wa ndani katika taasisi zao.

Naye Mkaguzi Mkuu wa ndani wa benki ya CRDB nchini Burundi Aloyce Leonard amesema wakaguzi wanatakiwa kuwa na uwezo wa kutoa uhakiki katika taasisi kulingana na mabadiliko ya teknolojia yanavyokwenda na kuendana na teknolojia mpya  ambapo mkutano huo wa 7 unafanyika jijini Arusha kwa siku nne na umejumuisha mataifa mbalimbali barani Afrika ikiwemo nchi ya Tanzania.

 

Previous articleMADIWANI WAASWA KUWA DARAJA KATIKA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI 2020-2025.
Next articleNEEC YAWAHIMIZA WAFANYABIASHARA GEITA KUKITUMIA KITUO CHA UWEZESHAJI KILICHOPO MKOANI HAPO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here