Home LOCAL KATIBU MKUU WA CCM CHONGOLO AANZA DODOMA ZIARA YA KUJITAMBULISHA

KATIBU MKUU WA CCM CHONGOLO AANZA DODOMA ZIARA YA KUJITAMBULISHA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akivishwa skafu alipowasili Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma leo, tayari kuanza ziara ya kujitambulisha kwa wana CCM na wananchi Mei 21,2021. Katibu Mkuu Chongolo na Naibu Katibu Mkuu, Christina Mndeme na baadhi ya timu ya sekretarieti yake wameanza ziara ya kujitambulisha kwa wanachama na wananchi ambapo leo ameanzia Mkoa wa Dodoma na Morogoro na kesho watakuwa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Tanzania Bara, Chritina Mndeme akivishwa skafu alipowasili ofisi ya CCM Mkoa wa Dodoma

Katibu wa NEC Organaizesheni, Mouldine Castico.

Waendesha bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM ulipokuwa unaanza Makao Makuu ya CCM  (Whitehouse)  jijini Dodoma leo.

Katibu Mkuu, Chongolo akiwapungia mkono wananchi alipowasili Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma kujitambulisha na kuongea na wanachama.

Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Mndeme wakitia saini kwenye kitabu cha wageni walipowasili Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Godwin Mkanwa.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka akitoa utambulisho baada ya Katibu Mkuu wa CCM na Naibu Katibu Mkuu, Mndeme kutia saini kwenye kitabi cha wageni.
Mkuu wa Mkoa mpya wa Dodoma, Anthony Mtaka akiwa kwenye kikao cha Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo na viongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma ambapo pia alijitambulisha. PICHA ZOTE NA RICHRD MWAIKENDA
Previous articleRAIS SAMIA APOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS WA BURUNDI EARISTE NDAYISHIME.
Next articleMAGAZETI YA LEO J.MOSI MEI 22-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here