Home LOCAL JESHI LA POLISI MKOA WA KAGERA LAENDELEA NA UCHUNGUZI NA KITU KILICHODAIWA...

JESHI LA POLISI MKOA WA KAGERA LAENDELEA NA UCHUNGUZI NA KITU KILICHODAIWA NI BOMU KUWALIPUKIA WATOTO

Na:Silvia Mchuruza, Biharamuro,KAGERA.

Jeshi la polisi mkoani Kagera linaendelea kufanya uchunguzi wa vifo vya watoto wawili vilivyotokea wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera baada ya kulipukiwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.

Akizungumza na waandishi wa habari mei 28 mwaka huu  Kamanda wa Polisi mkoani humo, Revocatus Malimi amewataja watoto hao kuwa ni Daniel Joseph (14) na Charles Njora (16) waliofariki Mei 27, 2021 wakati wakichunga ng’ombe.

Ameeleza kuwa waliokota chuma na kuanza kukichezea lakini kililipuka na kusababisha vifo vyao.

“Tunafanya uchunguzi ili kubaini kama chuma hicho kilikuwa ni bomu na kilifikaje katika maeneo hayo. Watoto hao walikuwa wakijiandaa kurejea nyumbani baada ya kumaliza kuchunga mifugo.”

“Hawakujua, walipokiona chuma hicho walianza kukichezea na kililipuka na kuwachana maeneo mbalimbali mwilini,” amesema.

Amewatahadharisha wazazi  wanapobaini watoto wao wanachezea vyuma ambavyo hawavitambui watoe taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here