Home LOCAL HOSPITALI YA MIRACOLO SEGEREA WAPIMA AFYA BURE.

HOSPITALI YA MIRACOLO SEGEREA WAPIMA AFYA BURE.

 

Daktari wa hospitali ya Miracolo akichukua damu kutoka kwa Wananchi waliojitokeza kuchangia damu katika madhimisho ya miaka mitano ya hospitali ya Miracolo (PICHA NA HERI SHAABAN)

Mmoja wa Wananchi akipima afya bure Segerea katika madhimisho ya miaka mitano ya hospitali ya miracolo (PICHA NA HERI SHAABAN)

Mmoja wa Wananchi akipima afya bure Segerea katika madhimisho ya miaka mitano ya hospitali ya miracolo (PICHA NA HERI SHAABAN)

NA: HERI SHAABAN, Dar es Salaam.

HOSPITALI ya MIRACOLO ya SEGEREA Wilayani Ilala wamewapima afya bure wananchi wa  Segerea na maeneo ya jirani katika wiki ya maadhimisho ya miaka mitano ya hospitali hiyo.

Huduma hizo za matibabu bure zimezinduliwa mwishoni mwa wiki  ambapo mamia ya wananchi walijitokeza kwa wingi kupima afya zao.

Akizungumza katika uzinduzi huo Dkt.Bingwa wa Watoto wa Hospitali ya Miracolo Anna Deogratius alisema wiki moja ya madhimisho ya miaka mitano kutoa afya bure  wamepunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa.

“Hospitali yetu ya Miracolo imezindua upimaji wa afya bure segerea ambapo pia kuanzia juni Mosi hadi Juni saba wananchi watatibiwa kwa  gharama za chini “alisema  Dkt Anna.

Alisema katika uzinduzi huo mamia ya wananchi wa Dar es Salaam na maneo ya jirani waliojotokeza kwa wingi katika kupewa huduma.

Alisema wananchi wengi wanaitaji huduma za afya lakini wengi wao wanakosa kutokana na Changamoto za maisha na ukosefu wa kipato.

Amewataka wananchi kujenga tabia za kupima afya zao kila wakati kwa ajili ya kujitambua.

Aidha Dkt,Anna alisema kuwa Katika utoaji huo wa huduma za afya bure   kwa wananchi waliweza kuwapima magonjwa mbalimbali yakiwemo Kisukari, uzazi wa Mpango ,Upimaji wa damu alama, presha, Afya ya kinywa na meno,VVU,wingi wa damu na magonjwa nyemelezi.

Amewataka Wananchi kujenga Tabia ya kupima kila wakati sio kula dawa bila kupima.

Kwa upande wake Afisa Tawala wa Hospitali ya Miracolo Jacqureen Sarakisa hospitali hiyo imeweka utaratibu wake endelevu itakuwa inawapima afya wananchi kila wakati.

Afisa Jaqreen alisema Dhumuni la kutoa hiduma kwa jamii kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusogeza sekta ya afya karibu na wananchi sambamba na kusaidia wananchi wasio na uwezo kupima afya.

Mwisho

Previous articleTAMKO KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA KUTOTUMIA TUMBAKU DUNIANI
Next articleRAIS DK. MWINYI AFANYA MAZUNGUMZO NA MCHEZAJI MAMADOU WA CRYSTAL PALACE YA UINGEREZA, IKULU, ZANZIBAR, LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here