Home LOCAL FCS YASHIRIKIANA NA TAASISI YA WAJIBU KUJADILI RIPOTI YA CAG DODOMA

FCS YASHIRIKIANA NA TAASISI YA WAJIBU KUJADILI RIPOTI YA CAG DODOMA

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bwana Francis Kiwanga akizungumza wakati wa kufungua wa Jukwaa la wakurugenzi Jijini Dodoma. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU, Bwana Ludovick Utouh akizungumza wakati wa kuwasilisha mada katika mkutano huo uliofanyika leo Mei 12 Jijini Dodoma.    

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bwana Francis Kiwanga (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh (kulia) wakisikiliza michngo mbalimbali na maswali kutoka kwa wadau walioshiriki kwenye mkutano huo Jijini Dodoma.

Wadau Mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, wadau kutoka CSOS na kamati za Bunge walishiriki kwenye mkutano huo. 

DODOMA..

Foundation for Civil Society (FCS) kwa kushiriana na WAJIBU Institute of Public Accountability kupitia Jukwaa la Wakurugenzi wa Asasi za Kiraia Nchini  kwa pamoja wamekutana Jijini Dodoma kujadili Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 Katika kuboresha utendaji kazi.


Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo ulioeashirikisha wadau mbalimbali  Mkurugenzi Mkuu wa Foundation for CIvil Societ Francis 

Amesema lengo la mkutano huo ni kuweza kupata uchambuzi wa Taarifa hiyo na kuweza kuchukua hatua ili kuboresha uwajibikaji na uwazi katika kuboresha  utendaji  kwa Serikali.


“Kila mwaka huwa tunakutana kujadili taarifa za ukaguzi wa hesabu za serikali lengo likiwa ni kuongeza nidhamu na kudhibiti ubadilifu wa rasilimali za Serikali na kupitia maajadiliano hayo tutakuwa na jambo moja katika kuimarisha utendaji kazi wetu”amesema Kiwanga.


Ameongeza kuwa kama Asasi za kiraia wamekuwa wakifanya kazi na Serikali ili kuwasaidia wananchi katika suala zima la uwazi na uwajibikaji  kwa maslahi mapana ya Nchi.


Akizungumza wakati wa kuwasilisha mada kwenye mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WAJIBU  Ludovick Utouh ambaye pia ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Mstaafu ambapo Taasisi yake ndiyo iliyofanya uchambuzi wa Ripoti hiyo amempongeza CAG Charles Kichere kwa Ripoti nzuri yenye jumla ya Ripoti 21.


Aidha amesema kumekuwepo na suala la kuongezeka kwa hati chafu na kwamba suala hilo linaonyesha kuwepo na shida katika suala la Mahesabu huku akieleza kuwepo kwa udhaifu katika ukaguzi wa ndani.


Hata hivyo aliwataka wananchi kuhakikisha wanaimarisha masuala ya uwazi na uwajibikaji katika kuikosoa Serikali.


MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here