Home LOCAL CHADEMA YATOA POLE KIFO CHA MBUNGE WA KONDE MHE. KHATIBU SAID HAJI.

CHADEMA YATOA POLE KIFO CHA MBUNGE WA KONDE MHE. KHATIBU SAID HAJI.

 

Na: Mwandishi wetu, ZANZIBAR.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Khatibu Said Haji Mbunge wa Konde kilichotea leo Mei 20 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Akiongea kupitia taarifa yake ya maandishi Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar Salum Mwalimu amesema kuwa Marehemu ameacha alama ya harakati za mageuzi na kutetea haki na masilahi ya Zanzibar na Wa-Zanzibari.

“Itakumbukwa hata mchango wake wa mwisho Bungeni katika Mkutano huu wa Bunge la Bajeti unaoendelea aliwazungumzia kwa kina Masheikh wa Uamsho wanaoshikiliwa kwa tuhuma za ugaidi akikumbushia madhila na  kupatiwa haki zao” Amesema Mwalimu.

“Kwa niaba ya familia ya Chadema Zanzibar, na viongozi wakuu wa Chama natoa pole nyingi kwa familia ya Marehemu, Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Mhe  Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Zanzibar Mhe.  Nassor Mazrui, wananchi wa jimbo la Konde, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai na wote wanaoguswa na msiba huu” Ameongeza Mwalimu.

Aidha amewataka Watanzania wote hususani Wananchi wa Jimbo la Konde, na familia kwa ujumla kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu Cha msiba. 

Previous articleMAJALIWA: WAHARIRI ZINGATIENI VIWANGO NA UBORA KATIKA UANDISHI WA HABARI..
Next articleRAIS SAMIA WA TANZANIA NA RAIS MUSEVEN UGANDA WATIA SAINI UJENZI BOMBA LA MAFUTA DAR.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here