Home BUSINESS WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUCHUKUA MKOPO KWA MALENGO

WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUCHUKUA MKOPO KWA MALENGO

DAR ES SALAAM.

Wajasiriamali wanawake wa Kata ya Keko wameshauriwa kuwa na malengo au wazo la biashara wanayotaka kuifanya kabla ya kukopa ili mikopo hiyo ikafanye kile kilichokusudiwa na si vinginevyo.

Ushauri huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bibi Beng’i Issa alipokuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wanawake Wajasiriamali waliopo Kata ya Keko.

Mafunzo hayo yamefanyika Katika Ukumbi wa New Omax uliopo Keko na yamefadhiliwa na Taasisi ya Vijana Light of Success na yatafanyika kwa muda wa siku mbili.

Katibu Mtendaji alisema kuwa mafunzo hayo yatawaongezea uelewa kwenye masuala ya Biashara na ujuzi vile vile yatasaidia kutanua wigo wa Biashara zao na hatimaye kukuza mtaji hivyo hawana budi kuyazingatia.

“Nawashauri msichukue mikopo bila malengo. Mikopo ni mizuri na inasaidia lakini ukichukua ikafanye kile ilichokusudiwa kufanya.” Alisisitiza Katibu Mtendaji.

Aidha aliwataka Wajasiriamali hao kufanya kazi kwa kushirikiana, wasaidiane kuinuana na kutatua changamoto zao wenyewe.

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Vijana Light of Success Zena Mlokozi alimshukuru Katibu Mtendaji kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji katika siku za usoni na Mambo mengine.

Previous articleMJASIRIAMALI EVAGLORY LWEBANGIRA ANG’ARISHA MAONESHO YA IBUKIE JIJINI DAR.
Next articleSP MWANGAMILO ATETA NA WAENDESHA BODABODA JIJINI ARUSHA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here