Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.
KATIBU wa Shirika la Dawa Asili na ulinzi wa Mazingira (TRAMEPRO) Bonivetura Mwalongo amewataka wataalamu wanaotoa huduma ya Tiba Asili nchini kuhakikisha wanaendelea kufuata ushauri na maagizo yanayotolewa na Taasisi zinazowasimamia ili kuepuka kujiingiza kwenye changamoto dhidi ya Serikali.
Wito huo ameutoa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara fupi ya kikazi ya kujionea ujenzi wa kituo cha Dawa asilia ambacho kinajengwa na mtaalamu mtabibu wa Dawa asili Seleman Mwamsumbwe chanika Mkoani humo.
Akizungumza mbele ya wanahabari Mwalongo alisema wamefurahishwa na kile ambacho kinafanywa na mtabibu hiyo kwani kinakwenda kumjengea heshima kubwa na yeye kama katibu wa TRAMEPRO anawasihi na kuwaomba wataalamu wengine kujenga vituo hivyo Kwaajili ya kufanya shughuli zao.
“Leo Kwa mara ya kwaza nimefakinikiwa kufika chanika na kwakweli aliyenileta hapa ni huyu ndugu Mwamsumbwe na kubwa zaidi nikuona mazingira ambayo anafanyia kazi zake na ujenzi wa kituo hiki “ alisema Mwalongo
Nakuongeza kuwa “Mwasumbe ni mwanachama wa Shirika la Dawa Asili na ulinzi wa Mazingira TRAMEPRO na ndio maana nimelazimika kufika hapa na kuona hali halisi hivyo nachoweza kusema nampongeza Kwa hatua hii kubwa ambayo inamfanya kuwa wa kisiasa zaidi.”alisisitiza Katibu Mwalongo .
Aliongeza kuwa Mtabibu huyo amethubutu kwani ni matabibu wachache sana ambao wanaweza kufikia hatua ambayo amefikia mtaalamu huyo Kwa maana ya kujenga kituo cha Tiba tena Kwa kujidunduliza Kwa kile kidogo anachokipata.
Alifafanua kuwa miaka 20 iliyopita ilikuwa ni ngumu kusimama hadharani na kuzungumzia Tiba Asili kutokana na mazingira kiasi kwamba hata watu walikuwa wanaifikia Tiba hiyo Kwa sili lakini leo kutokana nai maboresho yaliyofanywa Tiba hiyo imekuwa kimbilio kubwa la jamii na wananchi kwa ujumla.
Mwalongo aliongeza kuwa leo takwimu zinasema kuwa asilimia karibu 70 ya watanzania bado wanatumia Tiba Asili na asilimia karibu 80 Duniani pia wanapata huduma hiyo hivyo niwazi kwamba anachokifanya Mwamsumbwe kinakwenda kumuongezea umaarufu.
Hata hivyo alimtaka mtabibu huyo kutosita kutoa taarifa pindi anapokutana na changamoto katika kazi zake huku akimkumbusha kutunza mazingira ni sehemu ya shughuli za Shirika hilo.
Alifafanua kuwa wao kama Shirika limekuwa likifanya mikutano mbalimbali inayoshirikisha mamlaka za Serikali na lengo nikutoa elimu juu ya Tiba Asili na namna inavyoweza kuleta tija kwenye nchi yetu.
“Shirika hili linawanachama karibu Mikoa 15 hapa nchini na mbali ya kutoa Tiba Asili lakini pia tunakumbushana namna ya kulinda mazingira lakini pia kukua katika huduma ikiwa pamoja na kujenga vituo ,kliniki, na maduka kama leo hii unavyofanya Mwamsumbwe.” Alisema Mwalongo.
Kwa upande wake Mtaalamu huyo alishukuru ujio wa katibu huyo nakwamba amejisikia Mwenye bahati kutembelewa na kiongozi mkubwa kutoka kwenye Shirika Lao.
Alisema yeye katika shughuli zake tangu ameanza miaka 20 iliyopita amekuwa akijitahidi kufanya Tiba kwa weledi nakwamba hajawahi kukutana na changamoto yeyote na hivi sasa anaendelea kupata miongozo mbalimbali ya Serikali ili kuweza kutoa Tiba yake Kwa uhulu na uwazi zaidi.
Mwisho.