Home BUSINESS NIC: BIMA YA COMESA MKOMBOZI KWA WASAFIRISHAJI MIZIGO NJE YA NCHI

NIC: BIMA YA COMESA MKOMBOZI KWA WASAFIRISHAJI MIZIGO NJE YA NCHI

Mtaalam wa Bima ya COMESA Jamila Ntaru akizungumza kwenye mahojiano maalum juu ya Bima ya COMESA na namna inavyofanyakazi katika kilele cha sikuu ya wakulima nanenane Jijini Mbeya.

 Mtaalam wa Bima ya COMESA Jamila Ntaru (wa kwanza kulia) akiwa na Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Bima laTaifa (NIC) (wa pili kulia) na watumishi wengine wakijadiliana jambo wakati wa kuhitimishwa kwa Maonesho ya Nanenane Agosti 8,2022 Jijini Mbeya.

Mhasibu wa Shirika la Bima la Taifa CPA Hilal Seif akiwaelezea jambo baadhi ya wananchi waliofika kwenye banda la NIC katika maonesho ya Nanenane yaliyomalizika jana kwenye uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.

Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Yessaya Mwakifulefule kushoto akijadili jambo na baadhi ya watumishi wenzake wakiwa katika banda la shirika hilo kwenye maonesho ya Nanenane yaliyomalizika jana Agosti 8,2022 kwenye uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya.

Meneja wa Shirika la Bima la Taifa NIC mkoa wa Mbeya Bw, Justine Seni akipitia nyaraka za baadhi ya wateja waliofika katika banda la shirika hilo lili kupata huduma.

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)
Na: HUGHES DUGILO, MBEYA.

Shirika la Bima la Taifa (NIC) limezungumzia uwepo wa Bima ya COMMESA ijulikanayo kama (International Trade) inayohusisha magari yote yanayosafirisha mizigo kutoka Bandarini kuelekea katika nchi za jirani zilizopo katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) lengo likiwa ni kulinda vyombo vya moto ambavyo vinasafirisha mizigo kwenda nje ya Tanzania. 

Akizungumza kwenye mahojiano maalum wakati wa kilele cha sikukuu ya wakulima Nanenane iliyohitimishwa rasmi Kitaifa Agosti 8,2022 katika viwanja  vya John Mwakangale Jijini Mbeya, Afisa wa Bima kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC) Jamila Ntaru amezungumzia umuhimu wa uwepo wa huduma hiyo ambapo amesema kuwa magari yote yanalazimika kukata Bima hiyo ili kupata kibali cha kuvuka kwenda nchi jirani. 

“Hii ni Bima ambayo ipo sana katika mipaka yetu na kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda tumefungua mipaka zaidi kwa kuweka matawi yetu katika mipaka yetu yote ili iweze kuwahudumia wasafirishaji kwa haraka na ukaribu zaidi” amesema Ntaru.

Amefafanua kuwa awali Bima hiyo ilikuwa ikitolewa katika Ofisi za makao makuu zilizopo Jijini Dar es salaam pekee hali iyopelekea usumbufu kwa wasafirishaji na kuchelewa kufanya safari zao ndipo Shirikia liliona ipo tija kwa huduma hiyo kutolewa moja kwa moja katika mipaka ili kuwafanya wadau hao kupata huduma hiyo kwa haraka zaidi.

“Kule mipakani tunafanyakazi masaa 24 kwa sababu tunajua magari yetu yanayosafiri huwa yanatembea muda wote hivyo kwa kurahisisha hilo tunafanyakazi muda wote jambo ambalo limerahisisha sana kupungua kwa foleni mipani” amefafanua Ntaru.

Shirika la Bima la Taifa (NIC) liliweka kambi katika maonesho ya Kilimo Nanenane kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali kufahamu Shughuli za Bima zinazotekelezwa na la Shirika hilo.

Previous articleTASAC KICHOCHEO AJENDA YA 10/30, YAWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUTUMIA BANDARI
Next articleSUA YAIBUKA KIDEDE KWA TAASISI ZILIZOSHIRIKI KWENYE MAONESHO YA NANENEN KANDA YA MSHARIKI.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here