Home BUSINESS UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA (MKUMBI) UMEGUSA SEKTA ZOTE...

UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA (MKUMBI) UMEGUSA SEKTA ZOTE – MHE. KIGAHE

Kamati ya kudumu ya bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira leo tarehe 24 Oktoba, 2022 imepokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) ambao umekuwa ukijulikana kama “BLUEPRINT”.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Erick Shigongo (Mb) amesema kuwa kazi hii inayofanywa na Wizara katika kutekeleza Maboresho ya Mazingira ya Biashara Nchini BLUEPRINT ni nzuri na elimu hii inapaswa kusambazwa hadi vijijini ili utekelezaji wake usambae nchi nzima na wananchi waielewe.

Mhe. Shigongo ameongeza kuwa kama nchi tunapaswa kujiuliza kwanini Nchi jirani kama Rwanda na Kenya wamefanikiwa zaidi katika kuboresha Mazingira yao ya Biashara kutuzidi sisi.

Akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Wajumbe wa Kamati, Naibu Waziri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) Amesema kuwa utekelezaji  wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) umegusa sekta zote ambapo Maboresho hayo yanayoendelea kufanyika yatapelekea Nchi yetu kuwa miongoni mwa Nchi ambazo ufanyaji wake wa Biashara ni rahisi na hii imetokana na juhudi kubwa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amefuta kodi mbalimbali ambazo zilikuwa kero kwa Wawekezaji wetu.

Mhe. Kigahe amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imejikita katika kuhakikisha inaweka miundombinu wezeshi kama Umeme, Maji, Barabara, pamoja na mifumo yote ya Kieletroniki ili kurahisisha utoaji huduma kwa Wawekezaji.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu amesema kuwa kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) imewezesha wawekezaji wetu katika sekta ya Kilimo na Mifugo hasa kupitia Viwanda vyetu vimepata fursa ya kuuza nyama iliyochakatwa nje ya Nchi kupitia kiwanda cha Eliya Food na Tanchoice.

Awali akiwasilisha taarifa ya Mpango wa Maboresho ya Mazingira ya Biashara (MKUMBI), Mratibu wa Maboresho hayo Bw. Baraka Aligaesha amesema kuwa kazi kubwa imefanywa katika sekta zote na imesaidia kufutwa ama kupunguzwa kwa Tozo, Ada na Faini 232 ambazo zilikuwa zikitozwa na Mamlaka mbalimbali za Udhibiti.

Bw. Aligaesha amesema kuwa Sheria na Kanuni 40 zimepitiwa na kufanyiwa marekebisho pamoja na Taasisi zilizokuwa na Muingiliano wa Majukumu zimeunganishwa ili kuboresha mazingira ya biashara nchini.

Previous articleWANANCHI SONGWE WATAKIWA KUHESHIMU MAENEO YA HIFADHI YATAKAYOBAKI BAADA YA KUMEGEWA SEHEMU YA HIFADHI
Next articleMATUMIZI YA SIMU YAONGEZEKA  NA KUFIKIA MILIONI 51-TCRA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here